Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesema wizara hiyo imelazimika kusitisha malipo ya fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa muda wa wiki mbili ili kupisha zoezi la uhakiki wa wanafunzi hewa
Amesema hadi sasa wanafunzi hewa zaidi ya 2000 tayari wamebainika kwenye vyuo mbalimbali nchini na walikuwa tayari kupokea fedha hizo jambo ambalo ni hasara kwa serikali.
Prof. Ndalichako amesema, tayari amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha upya majina ya wanafunzi wanaostahili kupatiwa fedha hizo bila udanganyifu.
Amefafanua kwamba, wamegundua taarifa zilizopelekwa awali zilikuwa na udanganyifu hivyo serikali imelazimika kusitisha zoezi la upelekaji fedha kwenye vyuo hivyo.
Kwa upande wa wanafunzi ambao vyuo vyao vimefungiwa Prof. Ndalichako amesema tayari wametoa maelekezo ya kuwasaidia kupata haki yao muhimu ya kusoma na kusisitiza hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye atakosa msaada wa serikali
No comments
Post a Comment