Na Peter Mkwavila,DODOMA
WATANZANIA wamekumbushwa kuiunga serikali ya rais Dkt John Magufuli katika kushirikiana kwenye suala la ulipaji wa kodi ili kuimarisha uchumi kwa ajili ya maendeleo badala ya kuwepa .
Mchungaji Marcel Mushi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Mnadani Revival Temple Dodoma alisema hayo wakati alipokuwa akihubiri kwenye ibada iliyofanyika katika kanisa hilo.
Alisema suala la kulipa kodi hata ndani ya vitabu vitakatifu lipo na watu walikuwa wakilipa, hivyo hakuna sababu ya kukwepa kinachotakiwa ni kushirikiana na serikali ili kuimarisha uchumi huo kwa kulipa kodi hiyo.
Alisema kodi hizo zimekuwa zikiwezesha kuwepo kwa miundombinu mbalimbali kama vile ya maji,umeme,afya,barabara na majengo ya taasisi.
“Hivyo ni muhimu kuunga juhudi za ukusanyaji wa kodi,na tulinde kodi kwa kuwa zinatengeneza miundombinu mbalimbali ambayo ipo kwa ajili ya kuinua uchumi wa Mtanzania”alisema.
Akihubiri katika ibada hiyo aidha amewataka watanzania kutokukwepa kwenye uwajibikaji kufanya kazi zinazohusiana na shughuli za kimendeleo.kwa kuwa wasipofanya hivyo wanaweza kujiletea umaskini.
No comments
Post a Comment