TFF
YAMUONDOA SAANYA LIGI KUU BARA.
MAREFA waliochezesha mchezo namba 49
kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye
ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye
Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.
Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao
cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na
kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya
kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi
ishughulikie.
Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha
mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya
Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili
waweze kumpangia daraja lengine la uamuzi.
Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la
kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.
Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho
kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa
katika mchezo huo.
KATIKA
LIGI YA DARAJA LA KWANZA,
Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha
mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya
waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi
wake.
Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya
usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya
mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na
hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake.
Kutokua makini kulisababisha mchezo huo
kumalizika kwa vurugu.
Pia Klabu ya Coastal Union imepewa
adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja
ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia
Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.
kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya
Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha
ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya
African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya
waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.
NJE YA TANZANIA
MENDES
AMSAFISHA MOURINHO KASHFA YA KUKWEPA KODI.
WAKALA wa meneja wa Manchester United,
Jose Mourinho amesema mteja wake huyo alilipa zaidi ya kodi ya euro milioni 26
wakati alipoondoka nchini Hispania kuanzia 2010 hadi 2013.
Taarifa hizo ziliwekwa hadharani jana na
Gestifute, kampuni ambayo inasimamiwa na wakala wa Mourinho, Jorge Mendes.
Kampuni hiyo ya Ureno ilitoa taarifa za
kodi ya meja wake huyo baada ya vyombo vya habari vya Ulaya kuchapisha madai
kuwa kumekuwa na mchezo wa kukwepa miongoni kwa baadhi ya wachezaji wkaubwa na
makocha wakiwemo Mourinho, Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil.
Gestifute ambao pia ndio wanaomsimamia
Ronaldo tayari walishatoa taarifa zinazoonyesha kuwa mamlaka za kodi nchini
Hispania walishawakagua wateja wao hao na kuona hawana matatizo yeyote kwenye
ulipaji wa kodi.
MIDDLESBROUGH
YAIADABISHA CHELSEA.
KLABU ya Middlesbrough inadaiwa kutaka
kiasi kikubwa cha paundi milioni 35 kwa ajili ya Ben Gibson ili kuitisha
Chelsea. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa katika kiwango bora msimu
huu akisaidia vyema safu ya ulinzi ya klabu hiyo.
Meneja wa Chelsea Antonio Conte bado
anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi katika kipindi cha usajili wa dirisha
dogo Januari lakini sasa inadaiwa kuna uwezekano wa kushindwa kumuwania Gibson
kutokana na bei yake. Everton nao pia wanadaiwa kutaka kumuwania Gibson ambaye
alisaini mkataba wa miaka mitano na Middlesbrough mapema mwaka huu.
LAMPARD
KUKALIA BENCHI LA THREE LIONS.
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa
Uingereza na klabu ya Chelsea, Frank Lampard anatarajiwa kupewa nafasi katika
benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uingereza.
Taarifa hizo za kocha mpya wa Uingereza
Gareth Southgate kumtaka Lampard zimekuja saa chache baada ya taarifa rasmi
kuwa Sammy Lee ameachia rasmi wadhifa wake wa kocha msaidizi.
Southgate anataka kuunda jopo lake
mwenyewe na anaona Lampard kama mtu atakayemfaa katika benchi lake.
Lampard ambaye alistaafu soka la
kimataifa muda mfupi baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, ndio
kwanza ameondoka New York City FC kufuatia kumaliza mkataba wake.
BARCELONA KILA USHINDI NI HISTORIA.
KLABU ya Barcelona jana imeweka historia
mpya ya kuwa timu ya kwanza kucheza pasi nyingi katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya jana.
Wakiwa tayari wameshafuzu wakiwa vinara
w akundi C, Barcelona walishinda mabao 4-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach,
mabao yaliyofungwa na Lionel Messi na Arda Turan aliyefunga hat-trick.
Katika mchezo huo Barcelona walicheza
pasi 993 ikiwa ni nyingi zaidi kuliko timu yeyote toka rekodi hizo zilipoanza
kutunzwa katika msimu wa 2003-2004.
Mapema msimu huu, kipa wa Barcelona
Marc-Adre ter Stegen aliweka rekodi mpya katika La Liga baada ya kutoa pasi
zilizokamilika 51 kati ya 62 alizopiga dhidi ya Athletic Bilbao.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
MATOKEO YOTE
Matokeo
Jumanne
6 Desemba 2016
KUNDI
A
FC Basel 1 Arsenal 4
Paris Saint Germain 2 Ludogorets Razgrad
2
KUNDI
B
Benfica 1 Napoli
2
Dynamo Kiev 6 Besiktas
0
KUNDI
C
Barcelona 4 Borussia Monchengladbach
0
Manchester City 1 Celtic 1
KUNDI
D
Bayern Munich 1 Atlético Madrid
0
PSV Eindhoven 0 FC Rostov 0
TIMU ZILIZOFUZU RAUNDI YA
MTOANO YA TIMU 16:
Atlético Madrid*
Barcelona*
Leicester City*
Monaco*
Arsenal*
Bayer Leverkusen
Bayern München
Borussia Dortmund
Juventus
Manchester City
Paris Saint-Germain
Real Madrid
TIMU 7 AMBAZO ZINAWEZA KUFUZU
[NAFASI 4 ZIMEBAKI]:
Sevilla
Lyon
Porto
København
Benfica
Napoli*
Beşiktaş
TIMU AMBAZO ZIMETUPWA EUROPA
LIGI:
Borussia Mönchengladbach
Ludogorets Razgrad
Besiktas
Rostov
Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi
***Mechi
zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumatano
7 Desemba 2016
KUNDI
E
Bayer 04 Leverkusen v
Monaco
Tottenham Hotspur v CSKA
Moscow
KUNDI
F
Legia Warsaw v Sporting
Lisbon
Real Madrid v Borussia
Dortmund
KUNDI
G
Club Brugge v FC
Copenhagen
FC Porto v Leicester City
KUNDI
H
Juventus v Dinamo
Zagreb
Lyon v Sevilla
03/06/17:
Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
No comments
Post a Comment