Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu, amasema kuwa wito wa Umoja wa Mataifa wa kuitaka isitishe ujenzi wa makaazi eneo linalozozaniwa la Wapalesrina kuwa ni aibu.
Taarifa kutoka afisi yake imesema kuwa Israel haitaheshimu matakwa ya azimio hilo.
Ilisema kuwa Israel inasubiri kwa hamu kufanya kazi kwa ushirikiano na Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, kukabiliana na kile ilisema ni madhara ya azimio hilo.
Katika hatua isiyo ya kawaida Marekani ilisusia kupiga kura kwa azimio la Umoja wa Mataifa, hatua ambayo imewezesha Israel kukosolewa rasmi juu ya vitendo vyake nchini.
Azimio hilo linashutumu Israel kwa kuendelea kujenga kimabavu eneo linalotambuliwa kama sehemu ya Wapalestina.
Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 14 katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo linatambua kuwa hatua ya ujenzi ya Waisrael katika eneo hilo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu inatishia mpango wa usoni wa kuunda Taifa la Wapalestina katika mapatano yo yote ya siku za usoni juu ya taifa huru la Wapalestina.
Hilo ni wazo linaloungwa mkono na Utawala wa Rais Obama ambao ulifanya Marekani kubadilisha msimamo wake wa kawaida ambapo imekuwa ikitumia kura yake ya turufu kuzuia ukosoaji wa Israil.
Huu ni uamuzi uliochukuliwa baada ya kujadiliana na wandani wa Rais Obama kwa miezi kadhaa ambapo kutambua iwapo na jinsi Rais Obama angeweza kutangaza wazi msimamo wake juu ya uwekano wa kuwa na mataifa mawili katika eneo hilo kabla hajaondoka afisini.
Lakini mrithi wake, Donald Trump, ametangaza wazi kuwa ataunga mkono Israil na alimwomba Bwana Obama atumie kura ya turufu kuhakikisha kuwa Israil haikosolewi katika mswada huo.
No comments
Post a Comment