Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea wamefikia rekodi ya kushinda mechi 13 mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Stoke City katika dimba la Stamford Bridge.
Kipindi cha pili kilichokuwa na mpira wenye kuburudisha kilishuhudia goli tano zikifungwa ambapo Chelsea ililazimika mara mbili kuongeza goli ili iongoze.
Gary Cahill aliipatia Chelsea goli la kuongoza kabla ya mapumziko, lakini beki wa Stoke Bruno Martins Indi alisawazisha goli.
Willian aliifanya Chelsea iongoze tena lakini Peter Crouch akaisawazishia tena Stoke, hata hivyo Willian aliongeza la tatu na kisha baadaye Diego Costa akafunga goli la nne.
|
Beki Gary Cahill akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa |
|
Diego Costa akifunga goli la nne la Chelsea na kufanya matokeo kuwa 4-2 |
|
Bruno Martins Indi akifunga goli la kusawazisha la Stoke |
No comments
Post a Comment