Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MAGUFULI ATAMBA KUSHINDA KWA "TSUNAMI"
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

SIKU moja baada ya matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza kuonesha kuwa anapaa katika urais, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ametamba kupata ushindi wa ‘tsunami’.
Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni mjini Geita jana jioni, Dk Magufuli alisema hana shaka kuwa atapata ushindi mkubwa kwa sababu amejionea hali ya kukubalika miongoni mwa Watanzania katika mikoa 15 aliyopita tangu aanze kampeni Agosti 23, mwaka huu.
“Nitapata ushindi wa tsunami kwa sababu watu wanataka kuendelea na Tanzania yao. Huu ni mkoa wangu wa 15, nimeanzia Katavi, nimeona jinsi watu wanavyotaka mabadiliko, watu wamejitokeza kila mahali kunilaki na kunihakikishia ushindi.
“Ndio maana niliamua kutembea kwa gari, kutembea katika barabara mbovu, kwani uwezo wa kutembea na helikopta ninao, ningeweza kuja hapa kwa helikopta, lakini niliamua kutembea ili kujionea hali halisi, ili nikifika Ikulu nikumbuke shida za Watanzania na nikafanye kazi ya kuwatumikia,” alisema Dk Magufuli.
Awali, mgombea huyo alipokewa kwa kishindo mkoani Geita liliko Jimbo la Chato aliloliongoza kwa miaka 20. Licha ya maelfu ya watu waliojitokeza kwenye mkutano wake mjini Geita, vile vile katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Bukombe, Chato na Geita, hali ilikuwa hivyo.
Akiwa mjini Geita, Polisi walipata kazi ya kusimamia usalama kutokana na msongamano wa watu uliokuwa uwanjani hapo hali ambayo kuna wakati ilitokea tafrani iliyosababisha sehemu ya umati kwenye Uwanja wa Kalangalala, kukimbia ovyo bila kufahamu chanzo.
Katika maeneo mengine hususan kwenye mikutano iliyofanyika kwa nyakati tofauti Katoro (Geita) na Lunzewe (Bukombe), zilisikika sauti zilizopazwa zikisema yeye ndiye rais. Akihutubia mjini Geita, Magufuli aliwataka wananchi wawazomee mafisadi kwa kusema haooo, nao wakaitikia kwa kusema ‘haooo’.
Aidha, alisema wakati mwingine watu wanaichukia serikali kwa sababu ya watu wachache. Kuhusu huduma mbaya hospitalini, Magufuli alisisitiza kwa kusema atahakikisha dawa zinapatikana hospitalini na wakati huo huo watumishi wa afya watapata maslahi ya kutosha.
Akiwa mjini Katoro katika Jimbo la Busanda, alisema hachukii utajiri isipokuwa anachukia ufisadi ambao umechangia baadhi ya huduma kutopatikana ipasavyo. “Sichukii utajiri, lakini nachukia ufisadi,” alisema mgombea huyo na kufafanua kwamba ufisadi ndiyo umekuwa ukisababisha hata dawa zikosekane katika hospitali badala yake, wananchi wanaambiwa wakanunue kwenye maduka binafsi.
Magufuli ambaye amekuwa akiahidi kutatua kero mbalimbali ikiwamo kukomesha ushuru kwa wajasiriamali wadogo wakiwamo mama lishe, wafanyabiashara ndogondogo na waendesha bodaboda, anasema anafahamu mianya ya kuziba kuhakikisha fedha hizo zinanufaisha wengi.
Akiwa kwenye mkutano huo wa jana mjini Katoro uliohudhuriwa na maelfu ya watu, alisisitiza kuwa serikali yake itajenga mazingira yakusaidia wanyonge. Magufuli ambaye alisisitiza kuwapenda watu wote wakiwamo wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, hata hivyo alisema, kwake jambo la msingi ni kazi tu.
Alisema ni lazima kutengeneza mazingira ya kusaidia wanyonge. Alisema umasikini upo asilimia 28 na malengo yake ni kuhakikisha unapungua kwa kiwango kikubwa. Alisema akiwa serikalini miaka 20, amejifunza mengi.
Alisisitiza kuwa lazima hata zao la pamba liwe juu. Kuhusu viwanda mkoani Geita, alisema ipo haja ya kuvifufua ikiwamo vya kukamua juisi ili kutoa soko kwa zao la nanasi na atahakikisha manufaa wanayopata wachimbaji wakubwa, yanapatikana pia kwa wachimbaji wadogo.
Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM inasema watawapa wachimbaji wadogo teknolojia mpya, vifaa vya uchimbaji pamoja na kuendelea kuwarudishia maeneo ya uchimbaji. Alisema katika uongozi wa sasa wa Rais Jakaya Kikwete, yamerudishwa maeneo 25.
Chanzo HABARI LEO

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MAGUFULI ATAMBA KUSHINDA KWA "TSUNAMI"

No comments :