Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MWANAMKE AUWAWA BAADA YA KUBAKWA DODOMA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na John Banda, Dodoma

MWILI wa mwanamke  mmoja umeokotwa ukiwa umekufa katika kichaka kilichopo katika kijiji cha Iringa Mvumi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha Alibakwa na kisha kuuawawa na watu wasiofahamika.

Katika taarifa ya Jeshi la polisi iliyotumwa kwa vyombo vya habari ilionyesha kuwa tukio hilo lilitokea Juzi augost 10 saa 7:30 mchana mwaka huu, ambapo mwili wa mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa alikuwa na umri wa miaka 40 na kwamba jina lake limehifadhiwa kwa sababu maalumu.

Kamanda wa polisi mkoani humo Lazaro Mambosasa alitoa wito kwa wakazi wa  kijiji cha iringa mvumi na vijiji jirani kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kusaidia kuwafichua wahalifu hao mapema ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wakati huo huo Mahakama ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma imemhukumu Mkengela Mchechele [27] kwenda jela miaka 30, na viboko 12 ambapo wakati wa kutoka atalipa faini ya shilingi mil 1 baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka11 jina limehifadhiwa 

Kabla ya kusomwa hukumu hiyo na hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakam hiyo Mh. Marry Senapee, mwendesha mashitaka  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi KANDORO BABILE aliieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 29/3/2016 huko Kijiji cha MLALI – IYENGU Wilaya ya Kongwa na mkoa wa Dodoma baada ya kumkamata kwa nguvu mtoto huyo akiwa nyumbani kwake.

Hakimu Mkazi  mfawidhi wa Mahakama  MARRY SENAPAE alisisitiza kuwa anatoa adhabu hiyo ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hizo.

Aidha Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma alisema, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limejipanga vizuri kuhakikisha wahalifu wote  wanaotenda makosa wanakamatwa, upelelezi wa kina unafanyika ipasavyo kwa mujibu wa sheria na kuwafikisha mahakamani ili haki iweze kutendeka. 

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MWANAMKE AUWAWA BAADA YA KUBAKWA DODOMA

No comments :