Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MICHEZO ITAZAMWE KWA JICHO LA TATU.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MICHEZO ni afya, michezo ni ajira kubwa sana yenye faida kwa mwanamichezo, jamii, serikali.
1961 ni mwaka ambao Tanganyika wakati huo ilipata Uhuru, lakini tangu kipindi hicho hadi sasa, mafanikio yaliyopatikana hayaendani kabisa na umri huo. Naanza kwa kujiondoa katika upande wa kulalamika, na ninaingia katika upande wa kutoa mawazo yangu ambayo kama yatakuwa na tija basi yafanyiwe kazi.

Michezo yote lazima iwe na vipaumbele, lazima tuache dharau kwa kuona kuwa michezo ni kwa wanaopoteza muda, walioshindwa maisha, Serikali lazima ishiriki kwa asilimia 100 katika michezo hasa kwa timu za taifa zote kwa michezo yote ambapo wizara husika inatakiwa iwe na bajeti kwa timu za taifa za michezo yote.
Naomba nishauri watumishi wa umma lazima watambue kuwa michezo ni ajira tena iliyo rasmi, ninaposema watumishi wa umma namaanisha kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Mawaziri, makatibu wakuu wa mawizara, viongozi wote katika Idara zote za Serikali na sekta binafsi, wazazi na walezi. Viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo lazima waoneshe mipango yao ya kitaalamu kwa kushirikiana na wataalamu wa fani zote katika michezo.
Kuna tatizo moja katika nchi yetu tunalo ambalo kama hatutalifanyia kazi basi tutasindikiza miaka mingine 50 bila mafanikio, huku tukileta makocha wa kigeni ambao hawaendani na utamaduni wetu, lugha kuwa kigezo kibaya cha uelewa kwa wanamichezo wetu. Wanamichezo wetu ni lazima wawe na weledi, wawe na elimu ya darasani, elimu ya maarifa, elimu ya ujasiriamali, wanamichezo wetu lazima wajifunze lugha muhimu kama kiingereza, kifaransa, kijerumani, kireno, kitaliano, na lugha nyingine za kibiashara za kimataifa hii ikiwa ni pamoja na waamuzi wa kati, wasaidizi na makamishna.
Lazima wanamichezo wetu wajitambue kwa kujua kuwa michezo ni ajira rasmi inayotambulika popote duniani na inalipa kuliko kazi nyingine kwa sasa. Serikali yetu ikijipanga vyema inaweza kupata kodi kwa kupitia wanamichezo, mfano kukiwa na wanamichezo milioni 1.5 nchi nzima na kila mwanamichezo akawa anatoa kodi kwa mwezi Sh 10,000 serikali itavuna Sh bilioni 15 kwa mwezi ambapo kwa mwaka serikali inakosa kiasi cha Sh zaidi ya trilioni moja kwa hesabu zangu ndogo tu.
Tusiangalie kodi tu pia tuangalie vijana wangapi wataweza kufaidika na huduma ya afya kwa kuiingizia Bima ya Afya ya Taifa kiasi gani kwa mwezi ikiwa hao hao wanamichezo milioni moja na nusu wakitoa Sh 79,000 itapatikana zaidi ya trilioni ngapi ambapo wataweza kuzisaidia familia zao kwa upande wa afya pia, ambapo hapa hata serikali itaonekana imefanya jambo la msingi kwa wananchi wake.
Turudi katika mada yetu kuu sasa baada ya kuona faida za kipato, mashirikisho, klabu ziwe na weledi katika uongozi wa michezo na utawala wa fedha, pia kuwe na wataalamu wa masoko na matangazo katika michezo yote hata ikiwezekana kuwe na ‘Nyumba ya Michezo’ ambapo vyama na mashirikisho yote watakuwa hapo kwa ajili ya kupunguza gharama za ujenzi wa majengo mengi ambapo kuna vyama au mashirikisho yatashindwa kumudu gharama, hapa inatakiwa vyama vyote na mashirikisho yote yawe na ushirikiano kwa ajili ya manufaa ya wanamichezo, serikali na wananchi kwa ujumla.
Nashauri kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi makazini kwa kupitia mashirikisho yao kuwe na ulazima wa kuwasomesha walimu wa michezo na hata ikiwezekana kwenda kusomea nje ya nchi ili kwanza waone jinsi gani wenzetu wanafanya nini au walifanya nini hadi kufikia hapo walipo fika, kwa kusikia na kuletewa waalimu haitakuwa na nguvu sana. Na kwa wale ambao watapata nafasi ya kwenda kujifunza sio warudi na kuanza kujisifia wameona nini, tunataka wakirudi waandike taarifa zenye tija ambazo zitatuongoza sisi kuweza kuandaa na sisi michakato ya kuandaa viwanja na mambo mengine yote katika uongozi na utawala wa michezo kwa weledi.
Mashindano ya Umishumta, Umisseta, Umitashumta, Umivusta, Shimisemita, Shimiwi tunaweza kuwapata wanamichezo wa kuwakilisha nchi kwa sasa huku tukijiandaa vyema kwa miaka 10 ijayo katika kila mchezo. Mashirikisho ya michezo Tanzania kuna haja ya kuwa na taarifa jinsi gani mashindano yao yameendeshwa na wanamichezo gani wanafaa kwa michezo ipi ili kwa sasa tuweze kuwatumia wanamichezo hao kwa kila mchezo wakati tunaandaa wanamichezo washindani wajao.
Ni aibu sana pale ambapo kila tunachofanya tunaonekana kama kuna watu wamejinufaisha tu kwa kupeleka wanamichezo ili wapate walau fedha ya kula siku mbili tatu. Ninashauri kuanzia sasa viwanja vyote vya michezo yote vijengwe upya kwa awamu na kuvipandisha hadi vifikie hadhi ya nyota kuanzia nne, ili hata mwanamichezo ambaye anacheza katika uwanja huo aanze kupata uzoefu wa uzuri wa viwanja, mwanamichezo mwenyewe naye na hadhi ya nyota nne na hata akiwa anawaza kuwa mchezaji wa kimataifa wa kulipwa kweli aonekane ametoka kwenye eneo linaloendana na kazi anayotaka kufanya, sasa mtu katoka kiwanja hakijulikani hata mshabiki anakaa wapi kweli tutapata nafasi ya kuchukuliwa nje?
Hivi hatushangai kwa nini wanamichezo wetu hawachukuliwi nje! Maana huyo mchezaji mwenyewe anashangaa hapo alipo hajawahi kupagusa unadhani akili yake itakuwa inafanya kazi gani zaidi ya kushangaa kila kitu badala ya kufanya kazi iliyompeleka. Ninashauri kuwe na shule za vipaji maalumu kitaaluma na michezo ambapo wazazi, mashirikisho na serikali vitasaidiana kwa asilimia watakazopanga kuwasomesha watoto na kupata mazao yaliyo bora kielimu na michezo.
Kampuni zote katika nyanja zote ziingie mikataba katika michezo, sio hasara sana kufanya hivyo kwa kuwa wao nao wanajitangaza. Ikiwezekana kuwe na mfuko maalumu kwa kampuni, mashirika yote pamoja hata na wizara kuchangia na kufanya kitu ambacho wadau wote tutapanga kukifanya kwa mustakabali wa taifa letu.
Lakini jambo lingine kubwa nashauri sana kuanzia shule za msingi hadi klabu ni lazima tena lazima sana, kusomesha watu wa huduma ya kwanza, pia kuwe na madaktari wa klabu kuanzia ngazi ya shule, tutawapataje madaktari hawa ni vyema tukae na kujadili kisha wapatikane watu hawa ni jambo la msingi sana, lakini pia ni vyema kukawa na washauri wa saikolojia kwa wanamichezo, washauri wa vyakula kwa wanamichezo, wanasheria wa wanamichezo na wataalamu wengine.
Wanamichezo wawe na umoja wao ambao watakuwa wanapeana taarifa za msingi halafu wenyewe sasa watagawana kwa michezo ambapo watakuwa wana wakilishwa na viongozi wao kupitia vikao vyao rasmi watakavyokaa na kupanga mikakati inayotekelezeka. Madaktari wa michezo, wanasaikolojia wa michezo, wana lishe wa wanamichezo, wanasheria wa michezo, wataalamu wote wa michezo wawe na umoja wao ambao nao watapeana taratibu zao na maendeleo yao pamoja na changamoto zinazowakabili.
Tuhakikishe kila mchezo duniani unapata mwakilishi kutoka Tanzania kwa wanamichezo wote wa timu zote za walemavu wa jinsia zote, michezo ya wasichana, michezo ya watoto wa jinsia zote na rika mbalimbali, timu za wavulana na pia vifaa vya kisasa vipatikane pamoja na viwanja vyote vya mikoa kujengwa upya kama nilivyosema kwa kufikia hadi ya kuanzia nyota nne na kuendelea, pia kwa wale wenye uwezo wa kifedha wajenge viwanja vyao ili kuwa na timu zao kama Azam FC.
Michezo haikwepeki lazima tuwekeze ndugu zangu, siasa haihitajiki katika hili, magonjwa yamekuwa mengi sana sasa hivi mbaya zaidi wagonjwa ni vijana wadogo, sababu kubwa ni kukosa mazoezi, vyakula vinaliwa bila mpango, mbaya zaidi vyakula vyenyewe zimejaa dawa tupu. Sasa hivi imekuwa kawaida kukuta kuna michezo uwanjani, lakini hakuna mashabiki, hivi tunadhani Watanzania hawapendi michezo?
La hasha, inaonekana idara za matangazo na uhamasishaji hazifanyi kazi zao ipasavyo hii ni aibu sana, pia sio lazima kipangwe kiingilio kikubwa sana. Mfano Uwanja wa Taifa hata kama kiingilio kitakuwa Sh 2,000 kwa watazamaji 30,000 mapato yatakuwa Sh milioni 60, lakini kwa kuwauza wachezaji kama vile Mwadui FC inacheza na Ndanda FC basi wale wachezaji wao watangazwe na sifa zao ili watazamaji tuvutike kwenda kuona hizo sifa zao na hapo tunaweza kuwaona wachezaji wa timu ya taifa kwa kuwa nao hawatataka kupoteza sifa ambazo wanazo.
Nimetoa mfano wa mpira wa miguu, lakini kuwe na matangazo kwa michezo yote isiwe kwa mpira wa miguu, na matangazo yawe na tija sio ili mradi tu kutimiza wajibu. Wenzetu wanaheshimu kila jambo wanalolipanga na kulitekeleza kwa umakini na weledi wa hali ya juu huku wote wakipeana motisha kwa kila ngazi ya mshiriki.
Hatuwezi kuongelea ngumi huku hakuna viwanja vya ngumi, hatuwezi kuongelea riadha wakati hatuna maeneo yaliyopangwa kitaalamu kwa ajili ya kuwapata wanariadha wa aina zote, nikimaanisha kuanzia mita 100 hadi marathon, tufe, mkuki, kisahani, baiskeli na michezo mingine yote inahitaji maandalizi yenye tija huku kila mshiriki akijua wazi kuwa anaheshimika na ana thamani na anashiriki kwa mapenzi kutoka moyoni na ni ajira rasmi.
Kinachotuangusha sisi ni kuona michezo sio ajira rasmi, hivyo huwa tunashiriki ili mradi halafu tunatafuta ajira nyingine na tukipata hizo ajira nyingine tunaacha michezo. Ni vyema tuondokane na hulka hiyo. Watanzania tujiongeze kwa kufikiria ni jinsi gani tutafanya vyema katika michezo yote hapa duniani na kupata ajira kwa kupitia tasnia hii.
Mwandishi ni mchangiaji na msomaji wa gazeti hili.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MICHEZO ITAZAMWE KWA JICHO LA TATU.

No comments :