Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KIVUMBI LIGI KUU BARA.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2015-16 ulioanza kutimua vumbi wiki iliyopita, huku baadhi ya timu zikianza kwa kishindo na zingine zikichechemea.
Jumla ya timu 16 zinashiriki katika ligi hiyo, ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika. Yanga ndio bingwa mtetezi wa taji hilo huku Azam FC ilimaliza ya pili katika ligi iliyopita na ndizo zitawakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa na yale ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Mwanzo wa nguvu
Mabingwa watetezi Yanga, Azam FC, Simba, Mtibwa Sugar na timu iliyopanda daraja ya Majimaji ya Songea zenyewe zilianza vizuri ligi hiyo kwa kushinda mechi zote mbili hadi sasa. Hivyo timu hizo kila moja ina pointi sita lakini zimetofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa na ndio maana Yanga ni ya kwanza kileleni kwa sababu tu imefunga mabao matano na haijafungwa hata moja.
Azam wenyewe katika mchezo wa awali walishinda bao moja kabla ya Jumamosi iliyopita kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakati Simba ambayo msimu uliopita ilifanya vibaya, katika mchezo wa kwanza ilishinda 1-0 na wa pili ikashinda 2-0 dhidi ya Mgambo ya Tanga.
Timu zilizopanda
Pamoja na msimu huu kupanda timu tatu, lakini Majimaji ya Songea ndio iliyoanza vizuri zaidi kwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kushinda mechi zote mbili za mwanzo. Majimaji ilianza kwa kuifunga JKT Ruvu kabla ya kuiadabisha Kagera Sugar katika mechi zote zilizopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mwadui ambayo imepanda msimu huu ilianza vibaya kwa kufungwa na Toto Africans Mwanza, lakini katika mchezo wake wa pili kwenye uwanja wao wa nyumbani, timu hiyo iliibuka na ushindi na sasa iko katika nafasi ya saba kimsimamo.
Toto Africans baada ya kuanza vizuri ligi, ilijikuta ikipokea kipondo katika mchezo wake wa pili na hivyo kubaki na pointi zake tatu katika nafasi ya nane. African Sports wenyewe ndio hawana pointi hata moja baada ya kucheza mechi mbili na kufungwa zote, hivyo kuwa na mwanzo mbovu.
Zenye pointi tatu
Kuna timu nne ambazo zimeshinda mchezo mmoja kati ya miwili ya mwanzo baada ya kujipatia pointi tatu hadi sasa. Timu hizo ni pamoja na Mbeya City, Mwadui, Toto Africans na Kagera Sugar. Timu hizi hazijaanza vibaya wala vizuri sana lakini zinatakiwa kupambana ili kuhakikisha kila ligi inavyokwenda zinazidi kuwa na mwendo mzuri kwa kuibuka na ushindi.
Zinazoshika mkia
Timu tano hazijashinda mchezo wowote, hivyo hazijapata chochote na kuzifanya kushika nafasi za chini kabisa. Kufungwa mechi mbili mfululizo sio jambo dogo hivyo timu hizo kama zinataka kubadilika na kuwa katika nafasi nzuri na hatimaye kuendelea kuwepo, basi zig
Ligi hiyo si lelemama hivyo inatakiwa timu kugangamala na kupiga kiume ili kuhakikisha wanashinda katika mechi zijazo. Biashara asubuhi, huo ndio ukweli wa mambo na kama utapanga karata zako vibaya mwanzoni, basi unaweza kujikuta ukiteleza na hadi kuangukia katika daraja la kwanza.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KIVUMBI LIGI KUU BARA.

No comments :