Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ASANTENI STAR TV ,TFF TUMALIZE VISINGIZIO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limeingia mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni mia nne hamsini (450,000,000), na kituo cha luninga cha Star Tv kurusha matangazo ya Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL).
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru kampuni ya Sahara Media Group kwa kuamua kuwekeza katika mpira wa miguu nchini kwa kuamua kuonyesha ligi daraja la kwanza.
Malinzi ameviomba vilabu vya FDL kutumia udhamini huo kama chachu ya mafanikio na kufanya vizuri katika ligi hiyo itakayotoa timu tatu za kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (FDL) msimu ujao.
Aidha Malinzi amewaomba wamiliki wa viwanja vinavyotumika kwa michezo ya FDL kuviweka katika hali nzuri ya matunzo ili mechi zinazochezwa katika viwanja hivyo ziweze kuwa nzuri kiufundi na muonekano wa kwenye Luninga.
Jumla ya udhamini wa Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa ni shilingi bilioni moja na milioni mia tatu hamsini (1,350,000,000) ikiwa ni udhamini wa milioni mia tisa (900,000,000) kutoka StarTimes  mdhamini mkuu wa FDL na milioni mia nne hamsini (450,000,000) kutoka StarTv.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Sahara Media Group, Samwel Nyala ameishukuru TFF kwa kuwapa nafasi hiyo ya haki za matangazo kampuni yake kwa michezo ya Ligi Daraja la kwanza nchini (FDL).
 Katika kuhakikisha michezo hiyo inaonekana kwa wingi zaidi, Nyala alisema watafungua mkondo (Channel) ya Star Sports Plus itakayokua itakayokuwa inaonyesha michezo tu ikiwemo ligi daraja la kwanza (FDL).  
Akiongea kwa niaba ya vilabu ya ligi daraja la kwnza nchini (FDL), Asha Kigundula - Afisa habari wa klabu ya Friends Rangers ya jijini Dar es salaam, ameishukuru TFF kwa kuweza kuwapatia udhamini kwenye ligi, jambo ambalo litawapelekea kujiandaa na kufanya vizuri katika ligi msimu huu.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ASANTENI STAR TV ,TFF TUMALIZE VISINGIZIO

No comments :