Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » NYUMBA YA MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI JAMES MBATIA YATEKETEA KWA MOTO.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Nyumba ya makazi ya mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia imeteketea kwa moto siku ya Jumamosi, majira ya saa saba na nusu mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa huenda ni hitilafu ya umeme unaosemekana kukatika asubuhi na kurejea mchana kwa nguvu kubwa. 

Akizungumza na Channel TEN, kaka wa Mbatia, Felix Kessy amesema hadi sasa wanachoweza kueleza ni uharibifu uliotokea kutokana na moto huo, kwani hawakuwepo wakati wa tukio, ingawa anawashukuru majirani walioweza kuokoa baadhi ya vitu vya ndani.

Amesema ni mapema mno kuzungumzia aina ya uharibifu kwani atakayeweza kujua zaidi ni mkewe na Mbatia ambaye kwa wakati huo Channel TEN ilipofika, haikuweza kuzungumza naye kwa sababu alikuwa amepandwa na shinikizo la damu kutokana na tukio hilo.

Mkuu wa oparesheni hiyo kutoka kikosi cha zima moto na uokoaji kwa wakati huo nyumbani hapo sajenti Haji Madulika amesema kikosi chake kiliwahi eneo la tukio ingawa kutokana na ukubwa wa moto, walishindwa kuokoa baadhi ya vitu.

Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / NYUMBA YA MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI JAMES MBATIA YATEKETEA KWA MOTO.

No comments :