Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MTUNZA BUSTANI YA MATUNDA NA MITI DODOMA ANYANG'ANYWA ARDHI NA MANISPAA, BAADA YA KUKATAA FEDHA SHILINGI LAKI MOJA, AFISA MTENDAJI AJIBU MAPIGO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

picha kwa msaada wa mtandao
Na John Banda, Dodoma

Mtunzaji na muuzaji wa miche  ya bustani na matunda George Salia ameulalamikia uongozi wa kata ya viwandani manispaa ya Dodoma kwa kitendo cha kuvamia eneo lake na kumtaka kuondoka  bila kufidiwa chochote.

Akizungumza na Rasi fm katika eneo  hilo lililopo kati ya ukuta wa sabasaba na mahakama ya ardhi George Salia alisema kata ya viwandani  ilivamia eneo lake analotumia kuoteshea miche yake.

Salia alisema mwaka mmoja uliyopita aliombwa na Diwani wa kata hiyo Jafary Mwanyemba kuwa wajenge vyumba viwili vya maabara ambapo kabla ya ujenzi huo walikatakata  idadi kubwa ya miti yake na kubomoa vibanda vilivyokuwepo katika bustani bila  kupewa fidia yeyote.

Alisema aliambiwa atapewa shilingi laki moja akaikataa kwa kua hakujua ni ya nini lakini pia alishtushwa na ujumbe ulio mjia kutoka kwa uongozi wa kata na kumtaka aondoke katika eneo lilolobaki bila maelezo yoyote wala barua hali iliyomsababishia kutojua cha kufanya.

Alisema pamoja nakutafuta msaada katika maeneo mbalimbali ya ofisi za serikali alishindwa kuupata kutokana na wahusika kumchukulia hana akili vizuri  [amechanganyikiwa] kitu ambacho sio cha kweli.

“siwezi kukubali kwa sasa nimejipanga kwenda kwenye vyombo vya sheria iliniweze kusaidiwa kupata haki zangu”

Salia alisema walipo chukua eneo hilo aliendelea kufanya kazi zake kwenye eneo lilobakia ambapo hata hivyo amekuwa akipewa vitisho kutoka kwa  uongozi wa kata kuwa anatakiwa kuondoka kwenye eneo hilo ambalo limejengwa mabara ya shule ya Sekondari ya viwandani .

Hata hivyo George alisema serikali imlipe haki yake sitahiki  kwani hana sehemu ya kufanyia kazi zake za kila siku ambazo ndizo zinampatia kipato   cha kuweza kukidhi mahitaji yake ya kila siku

Akizungumzia madai hayo Afisa Mtendaji wa kata ya Viwandani Fanuel Laurence alisema eneo halali la George ni lile lililopo nyuma ya jengo la CCM Mkoa pembezoni mwa mfereji wa kupitishia maji machafu wa sabasaba

“mimi ni mtendaji wa kata si msemaji wa ardhi bali ufafanuzi  zaidi unatakiwa kutolewa na mamlaka zinazohusika zikiwemo  Manispaa  na CDA"alisema

"Lakini hata hivyo niseme eneo lile tulipewa na CDA kwa ajili ya ujenzi wa maabara na pale ambapo huyo mtu anapazungumzia sisi tunataka kujenga jengo la utawala  na yeye anatakiwa afanyie shughuli zake nyuma ya jengo la CCM mkoa ambapo alikuwa anafanyia kazi zake tangu zamani".ameongeza

 kuhusu shilingi laki moja tulikaa kamati ya ujenzi ya kata  tukakubaliana kupitia ushauri wa Diwani Mwanyemba tumpe ili iweze kumsaidia kuhamisha miche yake toka sehemu ya ujenzi kuisogeza panapostahili lakini alikataa na sisi hatukuwa na jinsi tukamuacha lakini haikuwa na lengo la kumhonga kwa sababu tulipewa kihalali”, alisema Mtendaji huyo

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MTUNZA BUSTANI YA MATUNDA NA MITI DODOMA ANYANG'ANYWA ARDHI NA MANISPAA, BAADA YA KUKATAA FEDHA SHILINGI LAKI MOJA, AFISA MTENDAJI AJIBU MAPIGO

No comments :