Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MCHUNGAJI AOMBA MSAADA WA HALI NA MALI KUWATUNZA WATOTO 135 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ALIOJITOLEA KUWATUNZA DODOMA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Picha si halisi ya picha, ni moja ya pich azinazowakilisha eneo hilo {chanzo library}

Na John Banda, Dodoma

MCHUNGAJI Yoram Isaka wa kanisa la Methodist lililopo Mbabala A manispaa  ya Dodoma amewaomba wahisani mbalimbali kujitokeza ili kusaidia kituo   cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la wanagalilaya.

Msaada unaohitajika kwenye kituo hicho ni chakula, nguo, vifaa vya shule zikiwemo sale, viatu na mahitaji binafsi ya wasichana.

Akizungumza na Jambo Leo kijijini hapo mchungaji huyo alisema kituo hicho cha wanagalilaya kina idadi ya watoto 135 ambapo wanaosoma msingi ni mia moja na waliopo sekondari 35.

Alisema kwa muda mrefu sasa amekuwa akijinyima kwa kuamua kujitoa na kuomba misaada katika maeneo mbalimbali akitembeza fomu za kuomba kuchangiwa ili apate chochote cha kumuwezesha kuwatunza na kuwalea watoto hao ambao wengine wanaishi majumbani wao.

Na changamoto kubwa ilikuwa mwaka jana alipokuwa akiwalipia ada wanafunzi hao lakini sasa anaishukuru serikali ya Magufuli kuondoa ada na michango mingine mashuleni ambapo sasa kubwa kwake ni Chakula na mavazi.

“karibuni ndugu mwandishi hapa ndiyo kituoni, kituo chetu kipo kilometa 25 toka mjini barabara ya iringa unachepuka Bihawana kwetu kama unavyoona watoto hawa wametoka shule muda mfupi uliyopita wengi wao wanafanya vizuri mashuleni lakini sasa kinachohitajika ni watu waweze kujitokeza na kunisaidia kwani ukiacha watoto hawa wengine wapo majumbani wakiwemo wazee wasiojiweza,

"Nawashukuru washirika wangu wakubwa chama cha Biblia ambao hivi karibuni wamekisaidia kituo magodoro ya kulalia watoto na wengine wote ambao wamekuwa wakinisadia kwa namna moja ama nyingine kubwa ninaomba watu wenye mapenzi mema wakisaidie kituo hiki kwa wao kuja hata kuniita walipo kufuata msaada maana watoto hawa hawana sehemu nyingine zaidi ya hapa kituoni".

"Kingine hapa hatuna majengo ya kutosha ndiyo maaana ya watoto wengine kuwa majumbani wakiishi na walezi ambao ni wazee pia wasiojiweza”, alisema

Aidha Mchungaji huyo alisema  tayari baaadhi ya vijana kutoka kituoni hapo wapo vyuo vya udakitari na Uwalimu.

Kwa upande wao baadhi ya watoto wakituoni hapo waliozungumza na jamb oleo walisema wanafurahia maisha na msaada mkubwa wanaoupata toka kwa mchungaji wao huyo na kusema kikubwa wanachokihitaji ni mavazi na chakula ili waweze kusoma vizuri

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MCHUNGAJI AOMBA MSAADA WA HALI NA MALI KUWATUNZA WATOTO 135 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ALIOJITOLEA KUWATUNZA DODOMA

No comments :