Na hivyo ndivyo ilivyo maana kwa muda sasa wamekuwa
wakifanya vizuri katika mashindao mbalimbali ya soka ikiwemo michuano ya Uefa
Champions League pamoja na La Liga, lakini pia miongoni mwao wapo wengine
wanaofanya vizuri na kuvut anoti nene pengine kuliko wao je! Unalifahamu hilo?
Fuatana name ujionee wengine wanaowafuata na wanaowatishia ufalme wao huo.
Hii ni List kuanzia nafasi ya 5 kuja hadi ya kwanza
5.Harry kane {dolla 99.74 milioni}
Kama utakumbuka ni kwamba katika klabu ya Tottenham
ya nchini England kuna wachezaji wawili waliowahi kuingia katika orodha ya
wachezaji wanaopokea mpunga wa maana kwa mwaka kupitia soka ambapo ni Luca
Modrich ambaye baadae alitimkia nchini Hispania katika klabu ya Real Madrid
pamoja na Gareth Bale ambaye naye kwa kitita cha rekodi pia alitimkia Real
Madrid baadae sasa ni zamu ya kijana huyu mwingereza ambaye sasa anashikilia
nafasi ya tano kati ya tano bora kwa thamani ya mkwanja duniani kwa wacheza
soka.
Swali ni je! Tutegemee kumuona timu gani tofauti na
Tottenham?
4.Christiano Ronaldo {dolla 124.54 milioni}
Ukilitaja jina hili unakuwa unamtaja mtu mmoja muhimu sana katika klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno.
Kwa sasa ameshuka kutoka nafasi ya kwanza na ya pili
katika misimu mitatu iliyopita hadi nafasi ya nne msimu wa 2015/16, pengine
inawezekana pia kutokana na mabadiliko ya kisoka na ujio wa wawekezaji tofauti
pia vijana wanaochipukia zote zinaweza kuwa sababu, kwa sasa anaingiza kiasi
cha dolla milioni 124.54 .
3.Eden Hazard {dolla 142.56 milioni}
Ukiitaja chesea hasa katika idadi ya magoli
waliyonayo hivi sasa pamoja na safu ya ushambuliaji huwezi kumuacha mbelgiji
huyu ajulikanaye kwa ufungaji kila awapo na nafasi ya kufanya hivo, licha y
akwamba msimu huu mambo hayajakaa sawa kwani hadi sasa hajapasia nyavu hata
mara moja huku akitoa assist mbili pekee, lakini anaongoza ndani ya kikosi hicho
kuwa na thamani kubwa zaidi ya wenzake huku kidunia akishika namba tatu mbele
ya CR7 na Harry kane.
2.Neymar Do Santos {dolla 166.82 milioni}
Wakati anajiunga na fc Barcelona june 3 mwaka 2013 akitokea
klabu y aSantos nchini kwao brazil kulizuka ubishi kama atamfunika Lionel Messi
au atakosa namba, pia magwiji wawili wa Argentina Diego Armando Maradona na Edison Arantes do Nascimento
maarufu kama {PELE} wakiingia kwenye mgogoro wa mabishano na kuvikonga vyombo
vya habari juu y amwanasoka gani atakuwa moto na kumfunika mwenzake.
Ubishi huo
umemalizika hapo jana mjini Zurich wakati Messi na Neymar walisimama kuwania
uchampion wa dunia ambapo Leo Messi alitawazwa kushikilia tuzo hiyo kwa mara ya
tano na kuwafunika au kuvunja rekodi na kujiwekea yake kabisaaaa.
Sasa ananyakua kiasi
hicho cha fedha nab ado anayo nafasi hata kushika namba moja kama ataongeza
bidii na iwapo messi atazubaa au kushuka kiwango japo ni parefu alipomuacha.
1.Lionel
Messi {dolla 273.88 milioni}
Unapotaja sifa ya mchezaji wa dunia ni lazima utaje
baadhi ya sifa ikiwamo ya mchango wa mchezaji katika kikosi chake cha taifa
pamoja na klabu anayoichezea, kwa upande wake messi anastahili kutokana na
uwezo alionao, kwanza ni mchezaji bora wa dunia mwaka uliopita alitangazwa, pia
aliiwezesha Argentina kutwaa nafasi ya pili katika kombe la dunia mwaka 2014,
tatu ameipatia klabu yake ya Barcelona taji la UEFA Championz league 2014/15,
kombe la klabu bingwa dunia akifunga koli moja dhidi ya Guangzhou Evergrande nchini
japani pamoja na kombe la la liga 2014/15.
No comments
Post a Comment