Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » R.I.P FIDEL CASTRO, DUNIA ITAKUKUMBUKA KWA MISIMAMO YAKO THABITI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Kiongozi wa Cuba Mwanamapinduzi Fidel Castro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika jijini la Havana. Kifo hicho kimethibitishwa kwenye taarifa iliyotolewa televisheni ya taifa nchini humo  na ndugu yake Rais Raul Castro.
Kiongozi Mkuu huyo wa Mapinduzi ya Cuba amefariki dunia majira ya saa nne usiku kuamkia le akiwa na umri miaka 90.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Fidel Castro alizaliwa Agost 13, 1926 ambapo amewahi kuwa mwanasiasa wa Kuba, mwanamapinduzi wa Kuba, Waziri Mkuu wa Kuba kati ya mwaka 1959 hadi mwaka 1976 na amekuwa Rais wa Kuba huru kati ya mwaka 1976 na 2008

Akiwa mwanasiasa wa Kuba Fidel Castro amekuwa amkifuata misimamo mbalimbali ya siasa za ulimwenguni haswa ule wa Marxist na Lenini na baadaye msimamo wa kimapinduzi wa Kuba.

Fidel Casto ameweza kufanya kazi kama katibu wa kwanza wa chama cha Kikomunisti cha Kuba kati ya mwaka 1961 na 2011, chini ya utawala wake ambao ulikuwa wa chama kimoja, Castro ameweza kusimamia misimamo yake kimataifa.

Fidel Castro ameweza kuwa katibu mkuu wa umoja usiofungamana na upande wowote ule kati ya mwaka 1979 na 1983 na mwaka 2006 na 2008.

Fidel Castro amekuwa akiamini katika kufanya mapinduzi ya mtutu wa bunduki iwe kwa Latino Amerika, Asia na Afrika. “Kuhoji juu ya mapambano ya silaha kuwa ndiyo njia pekee ya ukombozi ninaweza kujibu kuwa ndani ya hoja hii taifa letu hatuna budi, katika raia wengi wa Kuba na mataifa mengi ya latino Amerika, hakuna njia nyingine ya kujikomboa zaidi ya matumizi ya mtutu. Hii inaonekana kuyafaa ata kwa mataifa mengine ya Asia na Afrika.

Kila mara mabeberu wanatumia kila namna wakiyaunganisha majeshi yao kwa kila taifa kuzuia demokrasia ya mapinduzi. Wanawanyonga watu kwa vitanzi, vitanzi hivi vinaweza kukatwa kwa kutumia mapambano ya silaha tu. Wanamapinduzi hawatumii silaha kama njia sahihi ya kujikomboa bali, hii ni njia inayoeleweka kwa haraka na wakandamizaji.

Kwa hiyo raia wana njia mbili kuvumilia ukandamizaji au kupambana na adui kwa silaha. Ifahamike wazi kuwa adui huyu ana nguvu za uchumi na kila kitu ata tekinolojia. Mapambano yanajumuisha kutumia kila kitu mlichonacho haswa matumizi ya rasimalia watu.” Anasema Fidel Castro katika mahojiano na mojawapo wa vyombo vya habari akiwa msituni.

Fidel Castro alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Havana akawa wakili kabla ya kujiunga na siasa ya mapinduzi.
Castro aliongoza harakati ya upinzani wa wanamgambo dhidi ya udikteta wa jenerali Fulgencio Batista tangu 1953.
Hatimaye mwaka 1958 alishinda jeshi la Batista aliyelazimika kukimbia nchi tarehe 1 Januari 1959.
Hivyo Castro akawa kiongozi mpya wa Kuba hadi mwaka 2006.
Castro hakukubaliwa na Marekani, hivyo akajiunga na siasa ya Umoja wa Kisovyeti dhidi ya Marekani.
Aliongoza harakati yake kuwa chama cha kikomunisti akatangaza ukomunisti mwenyewe.
Hata baada ya kuporomoka kwa ukomunisti kote duniani (1989) aliendelea kutawala kwa kufuata mfumo huo.
Baada ya upasuaji alioupata mwaka 2006 alikabidhi madaraka kwa mdogo wake Raul Castro.
Ambapo hii leo tunazungumzia kifo chake baada ya hapo jana kutangazwa ujumbe duniani kote juu ya kifo cha mwanamapinduzi huyu wa kihistoria kutoka huko nshini Cuba akitajwa kufariki jana  Novemba ,25,2016.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / R.I.P FIDEL CASTRO, DUNIA ITAKUKUMBUKA KWA MISIMAMO YAKO THABITI

No comments :