Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIZI HAPA ZILIZOTOKEA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA LEO
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

TANZANIA
Wanaohusika katika msururu wa vikao vya mashauriano ya mgogoro wa Zanzibar ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein, ambaye ndiye mwenyekiti huku wajumbe wakiwa ni makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi, marais wastaafu Amani Abeid Karume, Jakaya Mrisho Kikwete, Ali Hassan Mwinyi, Dokta Salmin Amour Juma na makamu wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye ndiye mwakilishi kutoka upande wa CUF.
Zanzibar iliingia katika mgogoro wa kisiasa miezi miwili iliyopita baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi visiwani humo Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi kwa kile alichokiita ukiukwaji wa sheria na utaratibu wakati wa zoezi la upigaji kura.
bbcswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

SYRIA
Vikosi  vya  jeshi  la  Syria  vikisaidiwa  na  mashambulizi makubwa  ya  anga  vimesonga mbele  kuelekea  mji muhimu  wa  jimbo  la  kusini  la  Deraa leo baada  ya kukamata  kituo cha  karibu  cha  jeshi.
Jeshi  la  Syria  limesema  limerejesha  katika  udhibiti wake  kambi ya  jeshi  ya  brigedi  ya  82, moja  kati  ya vituo  vikubwa  kaskazini  ya  mji  unaoshikiliwa  na  waasi wa  Sheikh Maskin, ambapo  kukamatwa  kwake  na  waasi mapema  mwaka  huu kulitishia  kuzuwia  njia  za  kulipatia jeshi  hilo  mahitaji kwenda  upande  wa  kusini.
Jeshi  pia  limesema  katika  taarifa  kwamba  limekamata eneo  la  milima  ya Al Hesh, kaskazini  magharibi  ya Sheikh Maskin.  Eneo  hilo  la  milima linaangalia  sehemu kubwa  inayodhibitiwa  na  waasi  la  Deraa  magharibi.
Kwa  upande  wake Marekani  na  washirika  wake wameshambulia  maeneo  ya  kundi  la  Dola  la  Kiislamu kwa  mashambulio  31  ya  anga jana  katika  operesheni yao  ya  hivi  karibuni dhidi  ya  wanamgambo  hao nchini Iraq  na  Syria.
dwswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

IRAN
Iran imesema  leo imeingia  katika  siku  za  mwisho  za kukamilisha  jukumu  lake  chini  ya  makubaliano  ya kimataifa  kuizuwia  nchi  hiyo  katika  mpango  wake  wa kinyuklia baada  ya  kusafirisha  madini  ya  urani yaliyorutubishwa  kwa  kiwango  cha  chini  kwenda  Urusi.
Shirika  la nishati  ya  atomic  la  Iran  limesema  tani  11 za madini  ya  urani  zimepelekwa  Urusi  jana , hatua  ambayo waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani John Kerry amesema  ni  muhimu  chini  ya  makubaliano  hayo  ya Julai 14 kati  ya  Iran  na  mataifa  makubwa  sita.
Kwa  kufanya  hivyo  Iran  sasa  kwa  kiasi  kikubwa itapunguza  kiwango  kikubwa  cha  madini  hayo  ya  urani, ambayo  yalirutubishwa  kwa  kiwango  cha  juu, na ambayo  yangeweza  kutumika  katika  utengenezaji  wa silaha  za  kinyuklia, lengo  ambalo  jamhuri  hiyo  ya Kiislamu  inakana kutaka  kufanya.
Kerry  amesema hatua  hiyo  ya  Iran  kusafirisha  madini hayo  kwenda  Urusi  imesogeza  mara  tatu  muda itakaoweza  kuchukua  kutayarisha  madini  hayo  kwa  ajili ya  utengenezaji  wa mabomu  kutoka  miezi  miwili ama mitatu  na  kufikia  miezi  sita  hadi  tisa.
dwswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

UJERUMAN
Mahakama nchini Ujerumani, leo imemhukumu meya wa zamani wa Rwanda kifungo cha maisha gerezani, kutokana na mchango wake katika mauaji ya watu zaidi ya 400 mwaka 1994, wengi wao Watusti katika kanisa.
Mahakama ya juu ya kanda ya mjini Frankfurt, imesema Onesphore Rwabukombe mwenye umri wa miaka 58, Mhutu na meya wa zamani wa wilaya ya Mavumba, alikuwa miongoni mwa watu walioamrisha mashambulizi dhidi ya kanisa katika mji wa Kiziguro.
Rwabukombe alikutwa na hatia ya kusimamia mauaji hayo, kuita washambuliaji zaidi na kupanga utaratibu wa kuzisafirisha maiti na kuzitupa shimoni. Mahakama pia imeondoa uwezekano wa kumuachia mapema, ikisema alikuwa na mchango mkubwa  katika kupanga mauaji hayo ya halaiki.
Kanuni ya sheria za kimataifa inabainisha kuwa mauaji ya kimbari yanaweza kuadhibiwa popote duniani, na siyo tu katika nchi yalikotendeka. Rwabukombe amekuwa akiishi Ujerumani tangu mwaka 2002 baada ya kutoroka Rwanda na kutafuta hifadhi Ulaya.
dwswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
UFARANSA
Mashambulizi  ya  Waislamu  wenye itikadi  kali  dhidi  ya jarida  la  masihara  la  Charlie Hebdo  yameifanya Ufaransa  kuwa  nchi  ya  tatu  hatari  kwa  waandishi habari  mwaka  2015, ikiwa  nyuma  tu  ya  Syria na  Iraq.
Hayo  yamesemwa  leo  na shirika  la  waandishi  wasio  na mipaka RSF. Shirika  hilo  lenye  makao  yake  makuu mjini  Paris  limesema  katika  taarifa  yake  ya  mwaka kwamba  waandishi  habari  67 wameuwawa  duniani  kote mwaka  huu.
Katibu  mkuu  wa  shirika  hilo  la  RSF Christophe Deloire ameliambia  shirika  la  habari  la  Reuters kwamba  wengi wao ni  waandishi  waliouwawa ili  kuwazuwia  kufanyakazi zao.
Waandishi habari  wanane  waliuwawa  mjini  Paris Januari 7  wakati Waislamu  wenye  itikadi  kali  wakiwa  na bunduki  waliposhambulia  ofisi  za  jarida  la  Charlie Ebdo, shambulizi  la  kwanza  la  aina  hiyo  dhidi  ya  nchi  ya magharibi.
Dwswahili

GUINEA 
Shirika  la  afya la  Umoja  wa  Mataifa WHO leo limeitangaza Guinea  kuwa  haina  tena  ugonjwa  wa Ebola miaka  miwili  baada  ya  kuripuka, na kusambaza vifo  katika  mataifa  ya  Afrika  magharibi na  kuisukuma jamii ya  eneo  hilo  iliyoathirika  sana  katika  ukingo wa kuporomoka.
Taifa hilo ambalo ni moja  kati  ya  mataifa masikini  sana duniani, na koloni  la  zamani  la  Ufaransa lilipatikana  na mgonjwa  mmoja  ambaye  ni  mtoto  mchanga  ambaye alikuwa  mhanga wa  kwanza  wa  ugonjwa  huo, na maafisa  wa  afya  waliweza  baadaye  kuorodhesha  vifo 2,500.
Kiasi  ya  watu 11,300 walikufa  kutoka idadi  ya  wagonjwa 29,000  walioorodheshwa, kwa  mujibu  wa  shirika  hilo  la afya  ulimwenguni  ambapo  wataalamu  wengi  wanaamini ni  idadi  ndogo kuliko  athari  halisi iliyosababishwa  na ugonwa  huo.
dwswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

AFGHANISTAN
Rais  wa  Afghanistan Ashraf Ghani ameahidi leo kuitisha uchaguzi  wa  bunge  na  serikali  za  mitaa  mwaka  ujao, wakati  akijaribu  kutuliza mvutano  wa  kisiasa  ambao unazuwia  mapambano  ya  serikali  yake  dhidi  ya wapiganaji  wa  Taliban.
Muda  wa  mwisho  wa  bunge  ulipangwa  kumalizika Juni 22 mwaka  huu, lakini  uchaguzi  ambao  ulikuwa  ufanyike Aprili  umeahirishwa  kwasababu  ya  hofu  ya  usalama na kutokubaliana  juu  ya  vipi  kuhakikisha  uchaguzi unafanyika  kwa  haki baada  ya  uchaguzi  wa  rais  ambao umebishaniwa  vikali mwaka  jana.
Iwapo uchaguzi  huo  utafanyika  kama  ulivyopangwa , utafanyika  katika  hali  mbaya  kabisa  ya  usalama, ambapo kundi  la  Taliban  linatarajiwa  kuendeleza kampeni  yake ya mwaka  huu  ambayo  ilihusisha kuukamata  kwa  muda  mji  wa  Kunduz kaskazini  mwa nchi  hiyo.
dwswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

BURKINA FASSO
Takriban maafisa 20 wa kijeshi wamekamatwa nchini Burkina Faso baada ya serikali kutibua njama ya kumuachilia huru kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Septemba.
Maafisa mjini Ouagadougou wanasema kuwa serikali ilitibua njama ya kumuachilia huru jenerali Gilbert Diendere.
Vyanzo vya afisi ya waziri mkuu Isaac Zida vinasema kuwa , maafisa hao walikuwa na nia ya kuwaachilia huru washukiwa wote wa mapinduzi mbali na kukirejesha kikosi hicho cha kumlinda rais kilichopigwa marufuku kufuatia jaribio hilo la mapinduzi.
Aliachia madaraka baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa umma na viongozi wa kikanda.
Kikosi chake kilichokuwa kikimlinda rais kimehusishwa na njama hiyo mbali na madai mengine mengi ya ukiukaji wa sheria na kwa ukatili uliotekelezwa wakati wa utawala wa rais Compaoré.
Njama hiyo imetibuka katika siku ambayo taifa hilo linamtarajia rais mpya kuchukua hatamu leo.
Rais huyo mpya Roch Marc Christian Kabore amesema kuwa ''sheria itafwata mkondo wake''
Waziri mkuu Zida amesema ''Tumewatia mbaroni ilikutoa ilani kuwa njama kama hiyo hainabudi ila kutibuka''
Jenerali Diendere na Compaore, wanakabiliwa na tuhuma za mauji ya rais wa zamani wa taifa hilo Thomas Sankara.
Wamekanusha madai dhidi yao.
Bbcswahili
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIZI HAPA ZILIZOTOKEA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA LEO

No comments :