Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » ZIKO HAPA HABARI ZA KIMATAIFA ZA LEO..PITIA KESHO TAKUWEKEA NYINGINE
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

URUSI
Rais  wa  Urusi  Vladimir Putin  amesema  Uturuki itajuta zaidi  ya  mara  moja  kuhusiana  na  hatua  yake  ya kuiangusha  ndege  ya  kijeshi  ya  Urusi  karibu  na mpaka kati  ya  Syria  na  Uturuki, akiongeza  kwamba  hata puuzia hatua  ya  Uturuki  ya  kuwasaidia  magaidi.

Ameishutumu Uturuki  kwa  kununua  mafuta  kutoka  kwa kundi  la  Dola  la  Kiislamu, na  kuongeza  kwamba  hatua ya  Uturuki  kuiangusha  ndege  ya  Urusi  ni  sawa  na uhalifu  wa  kivita.

Katika  maelezo  yenye kulenga  mataifa  ya  magharibi, Putin  amesema  katika  hotuba  yake  ya  kila  mwaka  kwa taifa  hilo  kwamba  nchi  hazipaswi  kufanya  unafiki kuhusiana  na  ugaidi, ama  kuyatumia  makundi  ya  kigaidi kwa  maslahi  yao.

Rais Putin ametoa  wito  kwa jumuiya  ya  kimataifa  kuja pamoja  kupambana  na  ugaidi.

dwswahili
********************************************************

MAREKANI

Polisi  nchini  Marekani jana  imewatambua  washukiwa wawili, mwanamume  na  mwanamke , ambao wameuwawa  katika  majibishano  ya  risasi  na  polisi kufuatia  mashambulizi  ya bunduki ambapo  watu  14 waliuwawa  na  wengine  17  walijeruhiwa  jimboni Califonia.
Mkuu  wa  polisi  wa  mji  wa  San Benardino  Jarrod Burguan  amesema  polisi haiamini  tena  kwamba mshukiwa  wa  tatu  amekimbia na  kusema  wana  imani kwamba  watu  wawili  waliofyatua  risasi  katika  jengo ndio hao  waliouwawa.
Wa kwanza  ni  Syed Rizwan Farook , mwenye umri  wa miaka  28, mzaliwa  wa  Marekani na  wa  pili  ni Tashfeen Malik  mwanamke  mwenye  umri  wa  miaka  27.
Burguan amesema  Farook  alikuwa  ni  mfanyakazi  wa serikali  kwa  muda  wa  miaka  mitano kama mtaalamu  wa masuala  ya  mazingira  katika  idara  ya  afya.
Rais barack Obama ametoa  wito wa  kuchukuliwa  juhudi za  kupambana na matukio ya mauaji  kama hayo nchini humo.

Bbcswahili
**************************************************************

UJERUMAN

Kansela  Angela  Merkel  na  rais  wa  Afghanistan Ashraf Ghani  wamekuwa  na  mazungumzo mjini  Berlin  jana.
Majadiliano  yao  yalituwama  zaidi  katika  masuala  ya wakimbizi , ambapo  kansela  Merkel  amesema  kwamba Waafghanistan  wanaokuja  nchini  Ujerumani  wakitafuta hali  bora  ya  kiuchumi  watarejeshwa  nyumbani.
Ameongeza  kwamba  watu  ambao  bado  wako  nchini humo wanapaswa  kusogea  katika  maeneo  salama badala  ya  kuhamia  barani  Ulaya.
Zaidi  ya  Waafghanistan 140,000 wameikimbia  nchi  yao mwaka  huu  wakihofia  usalama  wao  na  mashambulizi ya  wanamgambo  wa  Taliban. Wengi  wa  wale walioikimbia  nchi  hiyo  wameingia  nchini  Ujerumani.
Akizungumza  katika  mkutano  na  waandishi  habari pamoja  na  rais  Ghani  wa  Afghanistan , Merkel amesema Ujerumani  itatimiza wajibu  wake  wa  kiutu kwa Waafghanistan ambao  wako  katika  hatari  kubwa kwasababu  wanafanyakazi na  majeshi  ya  kigeni  kama jeshi  la  Ujerumani.

Dwswahili
******************************************************************

ENGLAND
Ndege za kijeshi za Uingereza zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha.
Duru za serikali zimesema ndege hizo tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus.
Awali, wabunge nchini Uingereza walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397 wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika bunge la Commons.
Jumla ya wabunge 66 wa chama cha Labour waliunga mkono serikali huku David Cameron akipiata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa katika bunge hilo.
Waziri Mkuu huyo alisema amechukua “hatua ifaayo kuweka taifa salama” lakini wapinzani wake walisema hilo ni kosa.
Ndege nne za kijeshi ziliripotiwa kupaa kutoka kambi ya kijeshi ya RAF Akrotiri, Cyprus, baada ya kura hiyo kupigwa.
Ndege nyingine nne zilikuwa tayari kupaa kutoka kambi hiyo, ambayo imekuwa ikitumiwa kutekeleza mashambulio nchini Iraq.
Mbili kati ya ndege hizo nne aina ya Tornado zilirejea Cyprus saa tatu baadaye.
Taarifa zinasema jeshi la wanahewa la Uingereza, maarufu kama RAF, “limekuwa likijiandaa kuhusika katika mashambulio hayo, kujiunga na mataifa mengine ya muungano yanayokabiliana na IS nchini Syria, “kwa miezi kadha”.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn alipinga mashambulio hayo lakini chama chake kiligawanyika, baadhi ya viongozi wake wakuu wakijitenga na msimamo wake.

Bbcswahili
********************************************************************
SUDANI

Herve Ladsous, mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa amesema kuwa mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Agosti kati ya pande hasimu za Sudan Kusini yamefikia hatua nyeti.
Mapatano hayo yameshindwa kutatua tofauti kubwa zilizopo kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir wa nchi hiyo na waungaji mkono wa aliyekuwa makamu wake, Riek Machar.
Herve Ladsous ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mapatano yaliyofikiwa kati ya pande mbili hizo hasimu yanatekelezwa kwa mwendo wa kinyonga jambo ambalo linahatarisha amani na usalama katika nchi hiyo change zaidi barani Afrika.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine milioni 2.3 kulazimika kuishi kama wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo tokea ijitenge na Sudan.
Wakati huohuo Bani Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba mivutano na chuki za jadi zilizopo kati ya pande hasimu huko Sudan Kusini zinaweza kuzua wimbi kubwa la mauaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Watu wapatao milioni 4.6 wa nchi hiyo wanakabiliwa na baa la njaa na wanahitajia misaada ya dharura ya chakula ili kuwaepusha na maafa yanayowakabili.

Iribswahili

****************************************************************************

NIGERIA
Nigeria imepunguza faini kubwa ambayo ilikuwa imeipiga kaMpuni kubwa zaidI ya simu za mkononi barani Afrika hadi dola billioni tatu nukta nne.
Kampuni hiyo ya Afrika Kusini MTN ilipigwa faini mwezi Oktoba baada ya kushindwa kuzima kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa kutoka kwa mtandao wake.
Faini hiyo ilimlazimisha mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo kujiuzulu na mauzo ya hisa ya kampuni kudorora.
Lakini kufuatia wiki kadhaa za majadiliano utawala umekubali kupunguza faini hiyo.
Faini hiyo ambayo inahitaji kulipwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ni zaidi ya faida ya mwaka mmoja ya MTN nchini Nigeria.
Nigeria imekuwa ikilazimisha makampuni ya mawasiliano kuwasajili wateja wao kutokana na hofu kuwa, kadi ambazo hazijasajiliwa zinaweza kutumiwa na makundi ya kigaidi na wahalifu.
BBCSWAHILI

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / ZIKO HAPA HABARI ZA KIMATAIFA ZA LEO..PITIA KESHO TAKUWEKEA NYINGINE

No comments :