Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » CDA, WAKAAZI MKALAMA WATIFUANA,KISA UPIMAJI NA JANJA JANJA YA VIWANJA DODOMA....PITIA HAPA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Moja kati ya maeneo yanayogombaniwa huko mkalama
Na John Banda, Dodoma

WAKAZI zaidi ya 600 wa kitongoji cha mkalama kata ya makulu manispaa ya Dodoma waliokuwa wanaidai Mamlaka ya ustawishaji mji CDA fedha za fidia ya mashamba yao kwa kipindi cha miezi sita wameamua kuanza kuyatumia kwa madai kuwa mamlaka hiyo imevunja mkataba.

Wakiongea na waandishi wa habari katika Eneo hilo  lililopo pembezoni mwa Bwawa kubwa kiasili ambalo limedumu zaidi ya Muungo Mmoja la Mkalama  ambalo limezungukwa na vilima kadhaa walisema CDA wamezoea kuwatia wananchi umasikini kwa kuwanyang’anya mashamba yao na inapofika swala loa kuwalipa fidia inakuwa kiini macho.

hili ni moja ya alama ya mkalama {ni bwawa la mkalama}
Kwa upande wake Lenard Ndama alisema wameamua kuanza kuyatumia mashamba yao kutokana na kucheleweshewa fedha zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi 6 ambazo CDA walifanya makubaliano nao na kupima maeneo yao tangu  mwaka 2015 mwezi wa sita wakiahidiwa kuanza kulipwa lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika.

alisema wakati CDA walikuwa wakiyataka maeneo yao walikuwa wakiongea nao kwa lugha laini lakini baada ya kuwakubalia na kupima kilichijitokeza ni pamoja na kuwadharau na hata wanapofika ofini kwao kudai fedha hizo hukimbiwa na badara yake walinzi huwajibu kwa kashfa na kejeli.

Nae Moleni Charles alisema yeye kwa upande wake hata hiyo hela haimtoshi ikilinganishwa na ukubwa wa Eneo lake maa yeye aliahidiwa kulipwa laki nne kwa eneo lenye ukubwa robo tatu heka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa upimaji huo upande wa wenye mashamba  Issaya Mchiwa alisema CDA walianza kuthamini mashamba ya wakulima Arlili 28, mpaka June mwaka 2015 ambapo walitakiwa kuacha kuyatumia maeneo yao na kusubili malipo ambayo wangelipwa  kwa kipindi cha miezi Sita  na kinyume na hapo atakaye kiuka atakuwa amevunja mkataba
Mchiwa aliongeza kuwa kitendo kinachofanywa na mamlaka hiyo cha kuanza kuuza viwanja vilivyopimwa kwenye mashamba yao kwa matajili tena kwa bei ya 10,000 kwa square tofauti ambayo ni kubwa sana ukilinganisha na wao walitakiwa kulipwa 600 kwa urefu huo huo.

“wamevunja mkataba wao kwa kutotulipa mpaka miezi 6 imepita sasa tunarudi kuanza kuyalima mashamba yetu tunajua walisha pima hivyo wakija itawabidi kufanya uthamini upya na kupanga malipo tofauti nay a awali kwani yalikuwa madogo tulikuwa tumekubali yaishe lakini sasa hakitaeleweka.

Hapa tulipo CDA wamekuwa wakija na matajili wanawaonyesha viwanja katika mashamba yetu sasa tunasema basi wameshatusumbua vya kutosha kwa pesa ndogo kama  mimi hapa tu heka na nusu hata milioni haifiki wengine hapa laki tatu mpaka laki na nusu hivi mtu kama huyu ataweza kulipia kiwanja au anafanywa kuwa masikini jumla? Alihoji Mchiwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili alisema anashangazwa na kauli hiyo ya  mamlaka hiyo kushindwa kuwalipa wananchi fidia zao wakati wao wanaendelea kulipa na wameshalipa nusu ya wanaodai ambapo mpaka sasa wameshalipa 2.3 Bilioni kwa watu 2,320 kati ya 4394 wa maeneo ya Mkala na Mkonze.

Alisema mapaka sasa waliobaki ni watu 1600 ambapo zoezi hilo la ulipaji unaendelea na kwa kipindi cha mwezi mmoja mamlaka hiyo itakuwa imekamilisha na kulifunga  zoezi hilo ambalo linafanyika kwa awamu.

“ni kweli kuwa wapo watu 40 kati ya hao ambao wameleta barua za malalamiko wakilalamikia kupata malipo kidogo ukilinganisha ukubwa wa maeneo yao na hilo tunalifuatilia ili tuone jinsi ya kulitatua, hivyo wananchi wasubiri pia wawasikilize viongozi wao wa maeneo kwa cheki zinapotoka wanajulishwa ambapo mwezi wa pili tutalifunga zoezi hilo”, alisema   

Imeandaliwa na John Banda

Imehaririwa na denice J. Kazenzele

jan/25/2016

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / CDA, WAKAAZI MKALAMA WATIFUANA,KISA UPIMAJI NA JANJA JANJA YA VIWANJA DODOMA....PITIA HAPA

No comments :