Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene akiongea na waandishi habari mjini Dodoma |
Waziri Chawene na Mkurugenzi wa Elimu Msingi Abdu Maulid katika mkutano na waandishi wa habari |
>>waziri wa nchi ofisi ya rais tamisemi amefanya ziara ya kushtukiza
>> kugundua kuwepo jipu lililoiva
ni baada ya kukuta barua ya afsa elimu ikimuelekeza mwalimu mkuu kuchangisha michango kwa wazazi
DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini Kuusoma
kwa kuurudia ili wauelewe Waraka No 6 wa 2015 wa Serikali unaotoa ufafanuzi
kuhusu Elimu Bure kuanzia Awali mpaka kidato cha Nne ili kuepuka kufukuzwa kazi.
Waziri huyo aliitoa kauli hiyo
kwenye shule ya msingi ya Dodoma Makulu alipofanya ziara ya kustukiza mara
baada ya kupata taarifa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Janeth Justine
aliitisha wazazi na kuwaagiza kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi.
Chawene alisema alipofika shuleni
hapo alikuta tayari mwalimu mkuu
amepokea fedha Toka serikalini 1052,000 zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya mwezi
januari na bado hazijatumika lakini tayari wameshaanza kufanya mipango ya
kukusanya fedha kwa ajili ya Umeme, Maji na mlinzi toka kwa wazazi.
Alisema alilazimika kufika katika
shule hiyo ili kuweza kujionea Dhana ya Elimu Bale na kuona jinsi Fedha hizo
zinavyotumika na alipomuuliza mwalimu kuhusu Garama za maji, Umeme na mlinzi
akajibiwa kuwa haizidi laki mbili lakini anashangazwa na kitendo hicho
kinachofanywa na baadhi ya maofisa wa serikali ngazi ya Wilaya.
“Ninyi wenyewe mmejionea kwa mwalimu
kuwa ameshapokea zaidi ya milioni moja na badara ya kufikilia jinsi ya kuzitumia
lakini wao wana mawasiliano na ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ambayo
imewaandikia barua yenye maelekezo ya kuwachangisha wazazi fedha
Na katika hili niseme tu kuwa hawa
watendaji wameshindwa pengine kutafri waraka wa serikali no 6 wa mwaka 2015
unaotaka kila mwanafunzi asome bure mpaka ngazi iliyoainishwa lakini kwa
makusudi kuna watu hawataki kuunga mkono juhidi za serikali badara yake
wanakiuka kwa makusudi maelekezo yaliyopo, nasema katika hili lazima tutachukua
hatua kali na kabla ya hapo ni lazima nijilizishe kuwa nani na nani ni wahusika
ndiyo nichukue hatua”, alisema
Awali mwalimu mkuu wa Shule hiyo Janeth
Justine alisema aliitisha kikao cha wazazi ambacho aliwataka kucha fedha za
Maji, Umeme na Mlinzi ambacho kiliendeshwa na Diwani kama mwenyekiti na pia
Afsa mtendaji wa Kata ambacho anasema alipata maelekezo toka ofisi ya
mkurugenzi huku akionyesha barua iliyotoka kwa afsa Elimu Msingi wa Manispaa.
“nilijua kuwa Fedha hizi ndizo
zinatosha kuendeshea shule kutokana na maelekezo yaliyopo lakini nikapokea
barua hiyo yenye maelekezo ya kukutana na wazazi ili tukubaliane nini cha
kuchangia shuleni hapo, barua hii hapa na mimi nilisema lazima waniandikie kama
uthibitisho ili kikitokea chochote iweze kunisaidia”, alisema.
Mapema wakati msafara wa Waziri
Chawene ukiingia shuleni hapo wanafunzi walikuwa madarasani huku kukiwa hakuna
mwalimu anayefanya chochote lakini dakika chache baadae kila darasa lilikuwa
Bize kwa walimu wote kutoka kwenye Ofisi yao na kuanza kufundisha ambapo
mwalimu Mariamu Andrew anayefundishia la kwanza chini ya mti alikazana tofaiti
na wenzake waliokuwa madarasani
Imeandaliwa na John Banda
imehaririwa na denice kazenzele
23/january/2016
No comments
Post a Comment