Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MKAKATI WA MITI MIL. 10 KUPANDWA DODOMA WAWEKWA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Dodoma
 
MKOA wa Dodoma umejiwekea mkakati wa kupanda miti milioni 10 kwa ajili
ya utunzaji mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa alisema hayo juzi mjini hapa
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kimkoa uliofanyika
katika Chuo cha Serikali za mitaa cha Hombolo.

Alisema mkoa wa Dodoma unatarajiwa kupanda miti milioni 10, ambapo
kila Wilaya itapanda miti milioni 1.5.

“Tunahitaji miti kwa ajili yetu sisi na kwa ujumla wetu, miti inauzwa
kwa bei nafuu ambayo kila moja anaiumudu” alisema

Alisema uharibifu wa mazingira katika mkoa wa Dodoma ni mkubwa hasa
kwenye maeneo ya vilima.

Alisema mwaka huu mkoa wa Dodoma umepata mvua nyingi ni vizuri kutumia
fursa hiyo kwa ajili ya kupanda miti.

Aliagiza kila shule ya msingi na sekondari kuwa na vitalu vya kupanda miti 400.
“Hata kwenye mashamba binafsi miti ipandwe mashamba mengi ya Dodoma
hayana miti tofauti na mikoa mingine ambapo mashamba yanakuwa na miti”
alisema

Akisoma taarifa ya hali ya upandaji miti kwenye chuo cha Serikali za
mitaa cha Hombolo, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk Mpamila Madale alisema
chuo hicho kipo katika mpango mkakati wa kupamda miti kila mwaka jumla
ya miti isiyopungua 1,500 ili kuweza kuwa na miti mipya 7,500.
Alisema kwa miaka mitano iliyopita  2010-2015, Chuo kilipanda miti
jumla ya miti 6,000 sawa na asilimia 80 ya makadirio na kati ya hiyo
miti 5,100 iliota

Alisema katika kipindi hicho lengo halikufikiwa kutokana na sababu ya
ukame uliokuwepo mwaka 2015 ambapo chuo kilipanda miti katika maeneo
machache.

“Upandaji miti siku ya leo kwa mashimo yaliyoandaliwa ambayo ni zaidi
ya 1,600 Chuo kitahakikisha miti yote iliyopandwa inatunza na kuota
yote kwa asilimia 100” alisema

Ofisa Misitu wa Manispaa ya Dodoma, Eline Kizigha alisema zoezi la
upandaji miti katika mkoa wa Dodoma ytangu msimu wa mvua uanze mwaka
huu limekuwa likitekelezwa na wadau mbalimbali wanaojihusisha na
hifadhi ya mazingira kutokana na kuwepo kwa mvua ambazo zinaendelea
kunyesha hadi sasa.

Alisema tangu mwaka 2010 hadi 2015 jumla ya miti milioni 2.4 ilipandwa
kwenye maeneo ya shule ya msingi, sekondari, watu binafsi na taasisi
mbalimbali kama makanisa na vyuo kama Chuo cha Serikali za Mitaa na
Chuo Kikuu cha Dodoma.

Alisema  licha ya ukame mifugo pia huaribu ukuaji wa miti inayopandwa.
 
Mwandishi: John Banda
Mhariri:Denice J. Kazenzele
january 31/2016 {jumapili

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MKAKATI WA MITI MIL. 10 KUPANDWA DODOMA WAWEKWA

No comments :