Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » CCM ZANZIBAR YASIFU HOTUBA YA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzabar kimeipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli  aliyohutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita  ikielezea mafanikio ya siku mia moja za uongozi wa Kiongozi huyo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai  ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na Wanahabari hapo Afisini kwake, Kisiwandui mjini Unguja.

Amesema kwamba serikali ya awamu ya tano imeonyesha nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi, hali inayopelekea mamia ya Watanzania kuendelea kuiamini CCM kwamba ni chama cha wananchi wote kisichoongozwa kwa misingi ya matabaka.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar alisema hotuba  hiyo ya Dr Magufuli ilijaa kila aina ya uzalendo na nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania hasa wanyonge na kuonyesha dhamira ya kweli ya utendaji wa taasisi za umma  kwa manufaa ya wananchi.

“ Tunampongeza Rais wa Jamguri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Magufuli pamoja na wasaidizi wake,  kwa hotuba yake iliyojaa busara, hekima, ukomavu wa kisiasa na kuongeza kuwa ni dira ya mafanikio yaliyotukuka katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisisasa”. Alidai Vuai.

“Pia tunawaomba watendaji wa serikali na taasisi binafsi kuendelea kuwaunga mkono viongozo hao, ili Tanzania iweze kufikia nia yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati katika miaka michache ijayo, na hilo linawezekana endapo kila mtu atafanya kazi kwa uzalendo na weledi wa nafasi anayoitumikia.”. alikazia Naibu katibu Mkuu huyo.

Vuai alisisitiza haja kwa wananchi kuwa mstari wa mbele katika kubuni na kupanga mikakati itakayosaidi kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi na kamwe  halitakiwi kuchanganywa na itikadi za kisiasa.

Akizungumzia  suala la marudio ya uchaguzi mkuu wa uliopangwa kufanyika Machi 20, Vuai alisema ni uamuzi wa busara na wa kikatiba wa Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Zanzibar ya mwaka 1984 na kuongeza kusema hakika yeye hana mamlaka kisheria ya kuingilia maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kwani ni chombo huru kama vilivyo Tume nyengine za Uchaguzi duniani.

“Dkt. Magufuli ameweka wazi kabisa kuhusu kile kinachodaiwa ati kuwa ni mgogoro wa uchaguzi wa marudio kwamba hawezi kuingilia Maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ambayo ipo kikatiba na ina Mamlaka kamili kama  zilivyo Tume zingine za uchaguzi duniani, hivyo haitakiwi kuingiliwa na maamuzi yake”. Alifafanua Vuai.

Naibu Katibu Mkuu huyo, alivitolea wito vyomba vya habari hapa nchi kutopotosha umma hasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa marudio  ulitajwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.

VUAI alitoa wito huo kwa vyomba vya habari kufuatia baadhi ya magazeti kuandika habari za upotoshaji kuwa “vyama 10 vyaigomea Tume ya Uchaguzi Zanzibar  kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio Visiwani Zanzibar”.

Alisisitiza haja kwa wanahabari kutambua kuwa baadhi ya vyama vya UPDP na UMD vilivyotajwa kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio, havikuweka wagombea wake    katika uchaguzi uliopita hapo Oktoba 25, na kuvihusisha kutoshariki kwa uchaguzi wa marudio kinalenga kukuza idadi ya vyama na hivyo kufanya usanii mkubwa wa kisiasa.   

Vuai amevitaja vyama vilivyosimamisha wagombea ni 14 ambavyo ni CCM, CUF, SAU,TLP,ACT Wazalendo, ADC, TADEA, AFP, CHAUMMA, Demokrasia makini, DP, Jahazi Asilia, NRA na TLP.

Kupitia mkutano huo,  Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar, amewahimiza  wananchi wote wapenda amani na utulivu wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio Visiwani Zanzibar, kwani hiyo ni haki yao ya msingi kikatiba na kidemokrasia.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / CCM ZANZIBAR YASIFU HOTUBA YA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

No comments :