Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » UBOVU WA NISHATI Y AUMEME TZ: TANESCO LITAWALIPA WATAKAOUNGULIWA VITU VYAO KAGERA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) mkoani Kagera limesema liko tayari kulipa fidia kwa mteja yeyote atayepata madhara yanayosababishwa na kukatika-katika kwa umeme,iwapo itathibitika kuwa chanzo cha hitilafu ni shirika lenyewe.

Kauli hiyo kutoka shirika hilo mkoani humo imetolewa baada ya wateja wengi kulalamikia shirika hilo,kwa kile kinachodaiwa kukata umeme bila kuwataarifu na kuwasha umeme ghafla,hali inayosababisha wateja wengi kuunguza mali zao,ikiwa ni redio,Luninga,firiji n.k.
Akitoa ufafanuzi juu ya kero hiyo kubwa kwa wateja wengi hasa wadogo na wakubwa mkoani hapa,Mhandisi Mwandamizi kitengo cha Usambazaji wa shirika hilo mkoani hapa Felix Olan’g,amesema kuwa changamoto hiyo inatokana na ya wateja wengi kuongeza kwa matumizi ya umeme kwa kuongeza vifaa vingine vinavyotumia umeme tofauti na maelezo yao ya awali,ambavyo kila mteja ulazimika kuwa wazi wakati akiomba huduma ya umeme.
Hata hivyo,Olan’g amesema kuwa Tanesco iko tayari kumlipa mteja yeyote anayeweza kudai fidia halali,ikiwa atapata madhara yatakayothibika kusababishwa na shirika hilo,ilimradi madai ya vifaa vitakavyodaiwa kuungua viendane na maelezo ya awali yaliyotolewa wakati wa maombi ya huduma ya umeme.
Ameongeza kuwa mteja anapaswa kutoa taarifa kwa ya matumizi ya umeme wake hasa pale anapoongeza hitaji kwa kuongeza vifaa vingine katika nyumba yake kwani huduma inayotolewa na shirika inategemeana na matumizi ya mteja.
Hapo awali katika swali lililoelekezwa kwa Tanesco mkoa wa Kagera na Afisa Mwandamizi Idara ya Mafao kutoka shirika la hifadhi ya jamii(NSSF) mkoa wa Kagera Gerad Mkonyi,wakati kikao cha watendaji wa Tanesco na wateja wakubwa wa Umeme mkoani hapa,alitaka kujua kama shirika hilo(Tanesco)lina utaratibu wa kuwalipa wateja waliounguliwa vifaa vyao kutokana na tabia ya shirika la Tanesco kukata umeme na kuwasha bila taarifa kwa wateja.
Akijibu swali hilo Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Kagera Mhandisi David Mhando,amesema kuwa Tanesco haitahusika kamwe kulipa wateja wataounguliwa vifaa vyao kutokana na sababu itayobainika kusababishwa na mteja mwenyewe au wateja wengine.
Kikao cha Tanesco na wateja wakubwa wenye viwanda mkoani hapa kiliandaliwa kwa madhumuni kupata changamoto na kutafuta jinsi ya kuzitatua,huku kati ya wateja shirika hilo mkoani hapa ni 51,042 wateja 42 tu ni wateja wakubwa wa viwanda.
Kwa mujibu wa Mhasibu wa Tanesco mkoani hapa Leonard Mayunga wateja hao 42 wanachangia asilimia 41%ya pato la mkoa huku wateja wadogo na wa kati uchangia asilimia 59% tu.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / UBOVU WA NISHATI Y AUMEME TZ: TANESCO LITAWALIPA WATAKAOUNGULIWA VITU VYAO KAGERA

No comments :