Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » PAPA FRANCIS AHITAJI MABADILIKO JUU YA FAMILIA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amechapisha mwongozo mpya kuhusu maisha ya familia ambapo anahimiza kanisa litambue zaidi uhalisia wa maisha ya siku hizi.
Mwongozo huo ume kwenye waraka aliouandika akizingatia majadiliano ya mikutano miwili ya wakuu wa kanisa hilo kuhusu sera, maarufu kama sinodi.
Waraka huo ulisubiriwa sana na waumini takriban 1.3 bilioni wa kanisa hilo duniani.
Kicha cha waraka huo ni "On Love in the Family" (Kuhusu Upendo katika Familia) na haubadilishi mafundisho ya kidini ya kanisa hilo.
Lakini unafungua njia kwa maaskofu katika kila nchi kufafanua mafundisho ya kidini ya kanisa hilo kuambatana na utamaduni wa maeneo yao, mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema.
Papa Francis amewahimiza mapadri kutumia hekima na busara wakishughulikia “familia zilizoumizwa” na kuwa na huruma badala ya kutoa hukumu haraka.
Amekosoa ubinafsi ambao anasema umewafanya watu wengi katika nchi za magharibi kuthamini sana kutosheleza mahitaji yao binafsi badala ya mahitaji ya wake au waume zao katika ndoa.
Huku akiunga mkono kutolewa kwa elimu kuhusu ngono, amesema inafaa kuwa kwenye mfumo wa kutoa elimu kuhusu upendo.
Amesisitiza sana kuhusu ulezi wa kiroho na kuandaliwa vyema kwa watu kabla ya kufunganishwa kwenye ndoa kuhusu mahitaji ya maisha katika ndoa.
Kadhalika, amesisitiza kuhusu umuhimu wa mapadri kwenye parokia pamoja na watu wengine kuwaelewa vyema watu wengine na udhaifu wa binadamu.
Waraka huo ni matokeo ya kazi ya miaka mitatu.
Papa Francis alituma hojaji kwa familia maeneo mbalimbali ya dunia akiwaomba wamjulishe matumaini yao na wasiwasi wao.
Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma.
Kwenye mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi.
Masuala hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Ingawa bado ametoa wito kwa kanisa hilo kutowafungia nje wapenzi wa jinsia moja, waraka huo haujabadilisha msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu familia za wapenzi wa jinsia moja.
Amehimiza ushauri wa kidini wa heshima kwa watu hao, jambo ambalo halijakaribia kutambua familia za watu wa jinsia moja au ndoa za wapenzi wa jinsia moja kama walivyotaka watetezi wa haki za watu hao.
Waraka huo, ambao kirasmi hujulikana kama ujumbe wa papa kwa waumini umekuwa ukivuma sana mtandao wa kijamii wa Twitter kote duniani, wengi wakitumia kitambulisha mada cha jina lake la Kilatini, #AmorisLaetitia.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / PAPA FRANCIS AHITAJI MABADILIKO JUU YA FAMILIA

No comments :