Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » HIKI NDICHO KILICHOYAKUTA MABASI YA CITY BOY JANA NA KUSABABISHA WATU 30 KUPOTEZA MAISHA, PICHA ZA MAJERUHI WALIOFIKA HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA ZIKO HAPA PIA.......
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Dakitari Bingwa wa majeraha ya ajali na Mifupa Ibanzi Ernest akimpa pole mmoja wa majeruhi hao jana katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma
***************************************************************************************
Na John Banda, Dodoma
MIILI ya Marehemu  13 kati 28  waliyopoteza maisha kwa ajili ya ajali iliyosababishwa na Mabasi ya Kampuni ya City Boys zilizoletwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma zimetambuliwa huku zingine zikishindwa kutambuliwa kutokana na kahalibika vibaya huku ikiwa imeibiwa kila kitu.

Jana katika kijiji cha Maweni Tarafa ya Kintinku wilaya ya Manyoni mkoani Singida, mabasi aina ya Scania lenye namba za usajili T531 BCE lilokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lenye namba za usajili T247 DCD likitoka Kahama kwenda Dar es Salaam, ambayo yaligongana uso kwa uso.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Mjini hapa,Daktari Bingwa wa majeraha ya ajali na Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Dk.Ernest Ibenzi alisema jumla ya maiti 13 kati ya 28 zimeweza kutambuliwa na ndugu zao.

Aliwataja waliotambuliwa na ndugu zao kuwa ni John Lukanda,Ismail Bashe,Paulo Mfaume,Diocles Wajubigiri,Rabia Levis Lema,Levoso Izrael,Lesta Kanguru Exavely,Kefon Deus.

Alizitaja maiti zingine zilizotambuliwa kuwa ni za Paulini Meza,Deogratius Charles Mamunyu,Betty Zumbe,Jesca Lazaro,Leornard Chacha Nyantikela.

Alisema  walipokea jumla ya majeruhi 15 ambapo 7 waliwatibu na kuwaruhusu kurudi nyumbani huku 8 wakiwalaza kwa ajili ya matibabu zaidi.

‘’Tulipokea awamu ya pili  majira ya saa 6 usiku walikuja marehuhi wengine 8 huku wawili wakiwa wameumia vibaya sehemu za kichwa tuliwapeleka wodi mamba 11’’

‘’Ila watano tuliwafanyia operesheni ili damu zisiendelee kuvuja’’

Dk Ibenzi alisema kati ya wagonjwa hao wawili ilibidi wawapelekeChumba cha wagonjwa mahututi( ICU) kutokana na kuumia vibaya  sehemu za kichwa.

‘’Kati ya hao Wagonjwa  wawili tuliowalaza ICU, mmoja hatukumtambua kwani hakuwa na uwezo wa kuzungumza  jina lake lakini huyu mwingine tulimtambua kwa jina la Leornard Chacha ambaye amefariki leo (jana) majira ya saa 3 asubuhi’’  

Dk Ibenzi aliwataja waliolazwa katika hospitali hiyo na mikoa wanayotoka katika mabano kuwa ni,Katra Abbubakari(Geita), Athumani George (Morogoro), Jamilah Mathias(Geita).
Aliwataja wengine waliolazwa kuwa ni Mjaidi Mohammed Waziri(Kibaha) Monika Rabani (Dodoma),Disco Wabale(Dodoma)

 ‘’Majeruhi wanaendelea vizuri ila kuna wengine wapo Manyoni ila Dereva wa moja kati ya magari hayo ambaye alikuwa Manyoni alifariki muda mfupi mara baada ya kufikishwa hospitali’’

Alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo ni kucheleweshwa kwa majeruhi hali ambayo iliwapa wakati mgumu kwenye kuwatibu.

‘’Tulipokea maiti jana kuanzia saa 11 lakini cha kushangaza pamoja na Madaktari wetu na wahudumu kujipanga kwa ajili ya kupokea majeruhi na kuwatibu lakini tulijikuta tunawapokea wengine saa sita usiku hali zao zikiwa mbaya kutokana na kuvuja damu’’alisema

Alisema changamoto nyingine ni maiti zilishindwa kutambulika kutokana na kuharibika vibaya sehemu za kichwa huku zingine ubongo ukiwa nje.

FUNDI GARI AZUNGUMZA
Fundi wa gari lilokuwa likitoka Kahama kwenda Dar es salaam,Salum Mohammed alisema alimwambia dereva wa gari lao aendeshe taratibu na alimkanya kuhusiana na utaratibu wa kusalimia kwa kila mmoja kwenda upande wa mwenzake.

‘’Nilimkanya dereva wetu kuhusina na utaratibu wao wa kusalimiana kwa kila mmoja kwenda katika upande wa mwenzake lakini hakunisikiliza’’

‘’Katika moja ya safari zetu siku za nyuma alifanya hivyo nikamwambia hili litakuja kutugharimu siku moja lakini hakunisikia,sasa ndio limetokea wamesababisha vifo hivi’’alisema

MAITI ZA SACHIWA
kwa mujibu wa mmoja wa askari aliyekuwa akisimamia zoezi la utambuaji wa miili hiyo ya marehemu waliyotokana na ajari hiyo alisema zoezi hilo linakwenda kwa kusuasua kutokana na nyingi ya maiti hizo kufikishwa huku zikiwa zimeibiwa kila kitu

"miili mingine inashindwa kutambuliwa hasa hii iliyohalibika sana kutokana na miili hiyo kufikishwa hapa ikiwa imesachiwa na kuibiwa kila kitu kwa kuwa mifuko ya nguo zao ilikuwa imetolewa nje sasa haijulikani ni kina nani waliofanya mchezo huo kwa hakuna hata mmoja mwenye kitamburisho", alisema

MAJERUHI WAZUNGUMZA
Kwa upande wake majeruhi aliyelazwa wodi namba 11 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Mjaidi Waziri mkazi wa Kibaha alisema wakati ajali mikitokea  alikuwa amelala na alikuja kuamka mara baada ya kusikia kishindo.

‘’Nilikuwa nimelala nilikuja kustuka mlio mkubwa wa sauti,siamini kama nimepona ni ajali mbaya sana’’alisema

Naye Monika Rabani Mkazi wa Shelui Mkoani Singida ambaye amelazwa katika wodi namba  8 alisema alikuwa akisafiri  kutoka Dar kwenda nyumbani kwao Shelui.
Alisema katika safari hiyo aliongozana na mtoto wa Kaka yake aitwaye,Mohammed Hassan (2) lakini mpaka sasa hajui mtoto huyo yupo wapi.

‘’Sijui mpaka sasa mtoto wa kaka yupo wapi,ila ni ajali mbaya sana nimeumia mguu na kuvunjika huu mkono’’alisema

Kwa upande wake Disco Wabare  alisema alichokiona kabla ya ajali hiyo  ni madereva wa magari hayo kuwashina taa.
‘’Niliona wakiwashiana taa nilikuja kushtuka nipo hapa hospitali ila ni zaidi ya uzembe,uzembe wa madereva wamenifanya nipoteze jicho moja’’alisema

FAMILIA YATEKETEA
Akizungumza katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hosipitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,Said Musa alisema amempoteza baba yake mdogo,Peter Sinto mkewe Rose pamoja na mwanae ambaye hakutambulika jina lake.
Alisema Sinto alikuwa akitokea nyumbani kwao Tabora ambapo alienda kumtambulisha mkewe Rose pamoja na mwanae kutokana na kufunga ndoa mkoani Mbeya na wazazi kutokupata nafasi ya kuhudhuria ndoa hiyo.
Alisema Sinto alikuwa akirejea katika kituo chake cha kazi cha Mvomero kwani ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Mtibwa ya Mvomero Mkoani Morogoro.
‘’Inauma baba mdogo alitoka kujitambulisha nyumbani Tabora sasa alikuwa akirudi kazini kwake Mvomero kwani ni mwalimu tumewapoteza yeye mke wake na mtoto wake’’alisema

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / HIKI NDICHO KILICHOYAKUTA MABASI YA CITY BOY JANA NA KUSABABISHA WATU 30 KUPOTEZA MAISHA, PICHA ZA MAJERUHI WALIOFIKA HOSPITAL YA MKOA WA DODOMA ZIKO HAPA PIA.......

No comments :