Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » CHUO HATARINI KUMEZWA NA BAHARI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Katika Picha Eneo la Fukwe ya Bagamoyo upande wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni linavyotishiwa kuharibika vibaya kutokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.
SERIKALI imeiagiza Baraza la hifadhi ya Mazingira  (NEMC ) na Idara ya Mazingira  Ofisi ya Makamu wa Rais kufanya tathimini ya awali ya kuangalia ni namna gani itaweza  kuzuia maji ya bahari kuingia katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)  na kuharibu miundombinu yake ambapo hadi sasa takribani mita 70 hadi 100 ya bahari imeisogelea taasisi hiyo. 
 
Akizungumza  jana wilayani Bagamoyo,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina wakati wa ziara ya kutembelea Taasisi hiyo na kujionea ni namna gani bahari inavyosogea katika taasisi hiyo na kuanza kuathiri baadhi ya majengo.
Alisema  kutokana na hali hiyo kuwa ya dharura ameziagiza mamlaka hizo kufanya tathimini ya awali ambapo kufikia Januari 30 mwakani  watapaswa kukabidhi ripoti ya awali kwa  serikali na kujua nini kifanyike katika kunusuru taasisi hiyo na kuifanya mahala pazuri pa kujifunzia masuala ya utamaduni.

Mpina alisema ripoti hiyo itaweza kupelekwa serikalini ili mipango madhubuti  ianze kufanyika ya kuhakikisha taasisi hiyo inakuwepo na inaendelea kutoa mafunzo yake kama kawaida bila kuathiriwa na usogelewaji wa bahari katika maeneo hayo.

“Januari 30 mwakani tutapata hiyo ripoti na kuipeleka serikalini na kuangalia ni namna gani
tutakavyonusuru taasisi hiyo na kama kutahitajika utafiti mwingine wa kina kuhusiana na jambo hili utaweza kufanyika na kujua nini  kifanyike katika maeneo haya kama kutengeneza Makinga maji au Ukuta,”alisema Mpina.

Alisema hali ya bahari kuhamia katika maeneo ya nchi kavu  inatokana na kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi yanayotokea baharini ambapo kwa sasa  kina cha bahari kimeweza kuongezeka kufikia Sentimita 19 na kusababisha madhara ya maji kusogea katika maeneo ya nchi kavu.

Mpina alisema takribani majengo matatu ya taasisi hiyo yapo hatarini  kuathirika ambayo  yanajumla ya thamani ya kiasi cha sh.bilioni 1.6 ambapo yatasababisha hasara kubwa kwa majengo pamoja na taasisi hiyo.

Aidha  mpaka sasa kuna  baadhi ya fukwe tayari zimeanza kufanyiwa utaratibu wa kujengwa kwa 
kingo zikiwemo fukwe za Pangani Tanga,Kilimani Zanzibar,Kisiwapanza 
Pemba,pamoja na fukwe za 
Ocean road Dar es Salaam.  
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,Dkt.Herbert Makoye alisema taasisi yao inatatizo kubwa ya kusogelewa na bahari na kusababisha athari kubwa katika baadhi ya madarasa.

Alisema kwa sasa bahari inazidi kusogelea chuo hali inayotishia uwepo wa chuo hicho endapo jitihada dhabiti hazitaweza kuchukuliwa kwani hadi sasa uoto wa asili umeanza kutoweka kidogo kidogo.
  
Wakati huohuo,  Kufuatia malalamiko ya wakazi wa kata ya Bunju, Naibu Waziri Mpina alitembelea maeneo hayo yanayoathiriwa kwa kiasi kikubwa na maji ya mvua, na kuharibu miundombinu na mazingira na kupelekea afya za wakazi wa maeneo hayo kuwa hatarini kuathiriwa na magonjwa, Hali ambayo ilimlazimu Mpina kutoa agizo kwa NEMC, Idra ya Mazingira Ofisi ya Makmu wa Rais na Manispaa ya Kinondoni kufanya Tathnini ya mazingira katika eneo hilo na kuja na mpango mkakati wa muda mfupi na mrefu ili kuweza kunusuru hali hiyo.

Mpina aliwaasa wakazi wa eneo hilo pia kuzingatia ujenzi wa mipango miji na kuacha njia za maji na maeneo oevu

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / CHUO HATARINI KUMEZWA NA BAHARI

No comments :