Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » KUTUMBULIWA MKURUGENZI WA NIMR,SIO KWA ADHABU BALI ELIMU ILISTAHILI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Na.Mdede Musa Leonard
NIMR ndiyo taasisi yenye mamlaka kisheria kufanya tafiti za magonjwa hapa nchini,taasisi hii iko chini ya wizara ya Afya.

Ni Jambo la kusikitisha kama Taifa kuchanganya siasa na masuala ya kitaalamu
Utafiti hupingwa kwa Utafiti siyo Bla bla za kisiasa.

Rejea Kauli hizi;
“Ukweli ni kwamba ugonjwa wa Zika upo nchini kwetu na asilimia 15.3 ya watu waliopimwa wamegungulika kuwa na ugonjwa wa Zika”-Dr.Mwele Malecela,Mkurugenzi NIMR

“Ugonjwa wa Zika haujaingia Tanzania”-Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya
“Watanzania lazima wajikinge na Ugonjwa wa Zika”-Dr.Hamis Kigwangala,Naibu waziri wa Afya.

Dr.Mwele Malecela ndiye aliyesema ukweli kuhusu ZIKA kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa
Ni vema watanzania tukaelewa kuwa Mkurugenzi wa NIMR alitoa taarifa kuhusu uwepo wa ZIKA hapa nchini baada ya timu ya watafiti kuchukua sampuli miongoni wa watoto waliozaliwa na vichwa vidogo(Microcephaly) na mgongo wazi (Spina bifida) na kubaini uwepo wa VIRUSI VYA ZIKA kwenye sampuli hizo.

Binafsi nimeipitia ripoti kuhusu utafiti huo na kuona namna timu hiyo ya watafiti ilivofanya utafiti wao na kutoa majibu ya wazi kabisa

Ikiumbukwe timu ya watafiti hawa waliofanya utafiti huu si wa kutilia mashaka kwa kua wamefanya tafiti nyingi zenye tija hapa nchini ikiwemo ule utafiti wao uliopelekea kugunguliwa kwa aina mpya ya bacteria anayesababisha kuhara miongoni mwa watoto wadogo aliyepewa jina la “ENTEROBACTER BUGANDENSIS” utafiti huu ulichapishwa majarida mbalimbali ya afya ulimwenguni yakiwemo ya shirika la Afya duniani “WHO”.

Ni jambo la kutia simanzi pale kazi kubwa za kitafiti kama hizi zinapopotoshwa na kauli nyepesi za kisiasa.

Ieleweke wazi kutumbuliwa kwa Dr.Mwele Malecela wa NIMR ni mwendelezo wa vita ya wasomi na wataalamu kuwa wahanga pale wanaposema ukweli mambo ya kitaalam na kupingana na wakubwa zao kama ilivotokea kwa Bw.Lawrence Mafuru-msajili wa hazina.

Si kila kitu ni cha kupigia makofi,suala hili linatia doa taswira ya nchi yetu ktk medani za kimataifa, mashirika ya Kimataifa kama WHO hayawezi kushika kauli za kisiasa na kuweka kando utafiti huu,Tutegemee kuona mkwamo zaidi ktk sekta ya afya kama mashirika ya kimataifa kama WHO yatageuza mgongo kwa baadhi ya mipango na miradi ya kiafya hapa nchini......kwa upotoshaji.

Badala ya kutumia nguvu nyingi kukanusha ni vema wizara ya afya na serikali kwa ujumla itoe Elimu namna ya kujikinga na ugonjwa huu,kwani una madhara makubwa hasa kwa wajawazito na watoto walio tumboni mwao.

#copied+MussaMdede

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / KUTUMBULIWA MKURUGENZI WA NIMR,SIO KWA ADHABU BALI ELIMU ILISTAHILI

No comments :