Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MBUNGE WA KILOLO IRING AACHANGIA SHILINGI MILIONI 20
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Choo  cha mwalimu  mkuu  shule ya Msingi Mdeke  Kilolo

*************************************************************
MBUNGE wa  jimbo  la  Kilolo mkoani Iringa  Venance Mwamoto amechangia   zaidi ya Tsh milioni 20 kwa  ajili ya   kukamilisha miradi  mbaali  mbali  ya kimaendeleo  ikiwemo  ya  ujenzi  wa  vyoo vya  wanafunzi ,madarasa ,nyumba  za walimu na Zahanati  katika jimboni hilo  huku akiwataka viongozi  wa  serikali za  vijiji  na kata   kuhakikisha   wanakamilisha
ujenzi  huo kwa wakati na  ubora .

Pamoja na kuwataka   viongozi hao  kusimamia ujenzi   huo amesema atachukua hatua  kali  kwa  kiongozi  yeyote  wa serikali ya  kijiji ama kata ambaye atatafuna  fedha   hizo   za ukamilishaji  wa miradi hiyo ya kimaendeleo jimboni   humo.

Mbunge huyo  aliyasema   hayo  jana  wakati  alipofanya  ziara  ukaguzi  wa miradi  9  inayoendelea  kwa  nguvu  za  wananchi  na Halmashauri  ya wilaya   ya  Kilolo na  kueleza  kuvutiwa na  miradi  hiyo japo kunahitajika  msukumo  wa haraka  katika umaliziaji  wa miradi  hiyo hasa ile  ya vyoo vya  wanafunzi ili kuwawezesha  wanafunzi hao  pindi shule  zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.

Alisema kutokana na  hali ya  hewa  kuwa mbaya  kwa  mvua  kuchelewa  kunyesha katika  maeneo  mbali mbali ya  wilaya ya  Kilolo tofauti na miaka mingine ameona ni  vema   kuwapunguzia makali ya michango wananchi wake  na badala  yake  sehemu ya  michango  ambayo  walipaswa kuchangia  ili  kukamilisha miradi  hiyo  kuibeba  yeye  kupitia  mfuko wa  jimbo kwa  kuchangia fedha  hizo.

Kwani alisema ni rahisi  kwa wananchi  kuchangia  nguvu  zao  kwa kushirikia  katika  ujenzi  huo  wa miradi  hiyo  kuliko kushiriki kutoa  fedha jambo  ambalo kwa wananchi hao  ni  sawa na  kuwatesa kutokana na  wengi   wao  waliuwa  wakiishi  kwa kutegemea  kilimo na hadi   sasa matumaini ya  kupata fedha  kwa njia ya  kilimo yametoweka baada ya  mvua  kushindwa  kunyesha.

“Ninawaombeni sana  wananchi wangu  kwa sasa  ninyi  mshiriki  zaidi  katika maendeleo  kwa   kuchangia  nguvu  zenu  na mimi niwaunge  mkono kwa kuchangia  fedha  ili  kuifanya  miradi hii ikamilike  kwa  wakati”

Hata hivyo  alisema  kuna baadhi  ya maeneo wananchi  wanachangamoto  kubwa
ya  barabara hasa  zile  zilizopo  chini ya  Halmashauri  kuwa barabara  hizo  zitafanyiwa matengenezo na  ile  ya Tanrod kutoka makao makuu ya wilaya ya  Kilolo  hadi Ndiwili mpakani  mwa jimbo  la Kalenga  inaanza kujengwa  kwa  kiwango  cha lami  mapema mwakani  na kuwa kuanzia January  ujenzi   huo  utaanza kwani  barabara   hiyo  ipo
katika  ilani ya uchaguzi  ya CCM. 

Mbunge Mwamoto  alisema  kuwa kwa suala la  ujenzi  wa Zahanati na vituo  vya
afya  wananchi wamejitahidi  kwa maeneo mbali mbali aliyopita  kukagua
ujenzi  umefikia  hatua  nzuri  na  kutolea mfano ujenzi  wa Zahanati ya Masege  ambao jengo  lake   bado  kuezekwa na  nyumba  ya mganga ipo  katika  hatua  ya  kuanza  kupandisha  kuta kuwa kukamilika kwa Zanahati   hiyo  kutawawezesha  wananchi  hao  ambao  walikuwa wakilazimika  kufuata matibabu Kibengu na  Usokami  wilaya ya  Mufindi
wataweza  kutibiwa katika Zanahati   hiyo.

Alisema katika ziara  yake  hiyo aliyoambatana na  wajumbe  wa mfuko  wa jimbo
kupitia  fedha  za  mfuko wa   jimbo   Kijiji cha Mdeke ambako kuna ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia  Tsh milioni 1 na kwenye ujenzi wa  nyumba ya  mwalimu  amechangia  Tsh milioni 2 ,  sekondari ya Ipeta kwa  ajili ya  ujenzi  wa vyoo  vya  wanafunzi  amechangia Tsh  milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga amechangia Tsh  milioni  3 kwa ajili ya vyoo na nyumba  ya  mwalimu ,Wangama  amechangia  Tsh milioni 1 kwa  ajili ya ukarabati  wa madarasa ,Kitongoji  cha Ifiga amechangia Tsh milioni 1 kwa  ajili ya  kuanzisha mkondo  B wakati ujenzi  wa Zahanati na nyumba ya  Mganga  Masege amechangia  Tsh milioni 5

Mbunge Mwamoto  alisema ujenzi  wa  kituo  cha Afya  Ukumbi amechangia  Tsh milioni 2 na katika  ujenzi  huo nguvu  za  wananchi  ni Tsh milioni 35 na Halmashauri ni Tsh  milioni 10    huku  ujenzi  wa vyumba vyamadarasa  shule ya  Msingi  Italula amechangia Tsh  milioni 2  hata hivyo  alisema atafanya  ziara  ya ukaguzi  na uchangiaji  wa miradi ya  maendeleo  katika  jimbo zima ili  kupitia mfuko  huo  wa  jimbo miradi yote  iweze kupata  mgao   huo.

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MBUNGE WA KILOLO IRING AACHANGIA SHILINGI MILIONI 20

No comments :