Select Menu

function googleTranslateEl

HABARI KIMATAIFA

HABARI KITAIFA

Performance

Cute

My Place

MICHEZO

Racing

Videos

» » MAJAMBAZI MATATU YAUAWA DAR ES SALAM BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado hayajafahamika.

Alisema marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni 26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Hata hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na taarifa rasmi atazitoa leo.

Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Taarifa zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha, ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.
 
Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa  zaidi leo. 

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

/ / MAJAMBAZI MATATU YAUAWA DAR ES SALAM BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI

No comments :