Habari
Shughuli za kuaga mwili wa marehemu ziliongozwa na waziri mkuu
Mizingo Pinda pamoja na viongozi wengine akiwemo spika wa bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Anna Makinda naibu spika Job Ndugai,
mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Salma Kikwete, mke
wa waziri mkuu Bi Tunu Pinda pamoja na viongozi wengine wa chama na
serikali katika ngazi mbalimbali na wananchi wakiwemo wa jimbo la Ulanga
mashariki.
Akizungumza katika ibada ya misa ya kuuaga mwili wa Celina Kombani
mchungaji Wilfred Mmari amewasisitizia wanadamu kuhakikisha wanajiandaa
wakati wote kwa kutenda mema huku Bi Jenister Mhagama akizungumza kwa
niaba ya serikali amesema serikali itaendelea kutekeleza mipango yote
aliyoiacha waziri Kombani.
Kwa upande wake spika wa bunge Bi Anna Makinda amesema wanadamu
tunapaswa kushirikiana na makundi yote kwenye jamii kwa kuyatendea mema
huku katibu mkuu ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma Bw Habu
Mkwizu amesema marehemu Kombani katika uhai wake aliweza kushika nafasi
mbalimbali kwenye chama.
naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe wakiwemo wananchi
wawilaya ya Ulanga wamesema wamepeteza mtu muhimu ambaye aliwasaidi watu
wa aina zote na warika mbalimbali na ambapo ameweza kusaidia wananchi
wa jimbo lake katika makundi mbalimbali huku kwa upande wa watumishi
akiwezesha kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo makazi ya watumishi
ujenzi wa shule na kwamba hatua hiyo imewezesha kuvutia watumishi wa
serikali kufanya kazi wilayani humo.
Waziri Kombani alifariki Septemba ishirini na nne mwaka huu katika
hospitali ya Apollo nchini India alikoenda kupatiwa matibabu ambapo
aligundulika kuwa na kansa ya kongosho na kwamba marehemu ameacha
mjane, watoto watano na wajukuu wane, mungu ailaze roho ya marehemu
mahali pema peponi amani.
No comments
Post a Comment