Nahodha
wa Mbeya City Fc, Hassan Mwasapili amesema wachezaji wote ndani ya
kikosi chake wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara
dhidi ya Simba Sc ya Dar es Salam uliopangwa kucheza Oktoba17 mwaka huu
kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Akizungumza
na mbeyacityfc.com mapema jana, Mwasapili ameweka wazi kuwa huu ni
mchezo ambao City inautizama kwa macho matatu ili kufufua upya matumaini
yaliyofifia kutokana na matokeo mabaya kwenye michezo mitatu iliyopita.
“Tumejiandaa
vizuri, tunataka kushinda mchezo huu dhidi ya Simba ili kufufua upya
matumaini yetu kwenye ligi, tumekuwa na matokeo mabaya kwenye michezo
mitatu iliyopita, tulipoteza dhidi ya Azam Fc na pia Stand United na
tukapata pointi moja dhidi ya Toto Africans kufuatia sare ya bao 1-1
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ndiyo maana nadiriki kusema
huu ni mchezo ambao tunataka kushinda ili kulinda heshima yetu kabla ya
kutizama michezo mingine” alisema.
Akiendelea
zaidi nahodha huyo wa City alisema kuwa ligi ya msimu huu inachangamoto
nyingi kuliko ya msimu uliopita kufuatia kuwepo kwa ushindani mkubwa
kwenye kila mchezo unaochezwa dimbani akiwa na maana kuwa timu nyingi
zimefanya maanadalizi makubwa kuukabili msimu huu.
“Msimu
umekuwa na changamoto nyingi, timu zimejiandaa sana kuukabili ligi,
sisi hatukuwa na muda mrefu wa maandalizi lakini sasa tumeimarika, nina
imani kubwa mpaka mwisho ligi tutakuwa katika nafasi nzuri ya juu kwenye
msimamo, bado nia yetu ni kucheza mashindano ya CAF, na hili
linawezekana licha ya kuwa tumepoteza michezo minne hivi sasa”.
alimaliza.
City
inakuatana na Simba ukiwa ni mchezo wa tano kwa timu hizi huku kikosi
cha Msimbazi kikiwa kimeambulia kichapo mara mbili na sare mbili kwenye
michezo minne ya awali, mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa
ni kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo Simba ilikubali
kichapo cha mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na Rafael Daud na Peter
Mwalyanzi ambaye kwa sasa anacheza kwenye kikosi cha timu hiyo ya
Msimbazi.
Wakati
huo huo daktari mkuu wa City, Dr Joshua Kaseko amethibitisha kuwa nyota
wote ndani ya kikosi wako na afya njema na hakuna majeruhi yeyote na
kuweka wazi kuwa kwa ujumla hali ya kambi ya City kuelekea mchezo huo
wa tarehe 17 ni nzuri kabisa.
No comments
Post a Comment