Polisi nchini India wamewatia mbaroni watu sita baada ya mwanamume mmoja
Muislamu kupigwa hadi kufa kufuatia uvumi kuwa familia yake imeficha
nyama nyumbani kwao.
Mohammed Akhlaq alikokotwa kutoka nyumbani kwake Kaskazini mwa Uttar Pradesh na kushambuliwa na umati wa watu.
Mwanawe pia alijeruhiwa vibaya.
Kuchinja ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo wakaazi wake wengi ni Wahindu wanaoamini mnyama huyo ni mtakatifu.
Hivi majuzi Serikali ya chama cha Wahindu chenye mrengo wa kulia kimeweka sheria kali zinazopiga marufuku uchinjaji wa ngombe, uuzaji wa nyama na ulaji wake.

No comments
Post a Comment