Mgombea wa nafasi ya urais kwa kitiketi ya Chadema anayeungwa mkono
na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa
ameingia mjini Monduli kwa kishindo na kupokelewa na maelfu wa wakazi wa
jimbo hilo huku shughuli zikisimama kwa muda,
sikiliza hapa Mheshimiwa Lowasa akizungumza na wakazi wa monduli
https://www.hulkshare.com/4v5wongze4w0
Miaka 20 iliyopita ilikuwa ni ngome imara ya CCM lakini hii ni Monduli mpyaa kabisa.
Mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa akiwa mjini Monduli
amewaahidi kuhakikisha anakuwa mstari wambele katika kutetea na
kuimarisha maendeleo ya wanamonduli na watanzania kwa ujumla.
Awali akihutubia mikutano ya hadhara wilayani Monduli katika maeneo
ya Ingaruka, Loksari, Makuyuni na Monduli mjini amesema bado ni dhamira
yake kuona watanzania wananufaika na rasilimali amabzo zimewazunguka.
Akizunguma mara baada ya kukabidhiwa rasm kijiti cha kuwania nafasi
ya ubunge Bw Julias Kalanga amemhakikishia Edward Lowassa kuwa
atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo mjini Monduli.
Mgombea huyo wa nafasi ya urais na timu yake ya kampeni ameendelea
kupata uungwaji mkono na idadi kubwa ya wananchi ambapo kesho anatarajia
kuanza ziara ya kampeni zake mjini Same mkoani Kilimanjaro.
https://www.hulkshare.com/4v5wongze4w0
Waziri mkuu mstaafu anasemaje nae msikilize hapa
Kuhusu sera za Dk Magufuri na barabara anazizungumziaje nasari? msikie hapa chini
No comments
Post a Comment