Vitambulisho
134 vya Kupigia kura, vimekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa –TAKUKURU- mkoani Kagera baada ya kukutwa vimenunuliwa na Kundi
la watu kutoka kwa wapiga kura.
Taarifa
ambazo zimethibitishwa na Naibu mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John
Joseph vitambulisho hivyo vimekamatwa vikiwa tayari vimenunuliwa kutoka
kwa wananchi kwa bei ya kati ya shilingi 5,000 hadi 10,000.
Amesema
kuwa kukamatwa kwa Vitambulisho hivyo, kumetokana na baadhi ya Vijana
walioshawishiwa kuuza kadi hizo na kundi la watu wanaopita, kutoafiki na
kisha kulazimishwa kufanya hivyo.
No comments
Post a Comment