Wakati kukiwa kuna taarifa zinazoenezwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikisema mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jeneral Davis Mwamunyange amewekewa sumu na hali yake sasa hivi ni mbaya, huku taarifa hizo zikisema sababu ya kuwekewa sumu imetokana na masuala ya kisiasa,hatimaye Serikali imeibuka kwa mara nyingine na kukanusha taarifa hizo na kusema ni za uongo zenye nia ya kufakaranisha Taifa.
Akikanusha
Uvumi huo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa
habari, Afisa Habari wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya
Habari –Maelezo Assah Mwambene amesema Jeneral Mwamunyange yupo salama
na anaendelea na kazi zake,akidai kuwa taarifa hizo zinalengo la
kuchonginisha watanzania na jeshi na kuharibu picha ya Amani na utulivu
uliopo nchini.
Mwambene
amewataka Watanzania kupuuza taarifa hizo huku akiwasihi kutoingiza
siasa kwenye masuala nyeti ya nchi ikiwemo jeshi,kwani jeshi ni taasisi
isiyojihusisha na siasa.
Wakati
huo huo pia Serikali imetolewa ufafanuzi juu ya taarifa zilizoandikwa
kwenye Gazeti la Tanzania Daima ambazo zilikuwa zinaubeza uteuzi
uliofanywa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kwa kuwateua wakuu wa
wilaya wapya, wakidai uteuzi huo ulikuwa ni wakulipa fadhira kwa kwa
wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Akifafanua uteuzi huo, Mwambene amesema watu wanaobeza uteuzi huo watakuwa hawajui sheria za nchi na kufahamu mamlaka ya Rais.
Amesema
kwa mujibu wa sheria,kanuni za nchi na taratibu Rais anamamlaka ya
kufanya uteuzi wakati wowote inapobidi kwa malengo ya kuboresha
utendaji wa kazi serikalini.
“Serikali
imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na gazeti la Tanzania daima
kuhusiana na uteuzi wa Rais,taarifa hizi ni za kichochezi na zinalenga
kumchonganisha Rais na wananchi wake”amesema Mwambene.
Aidha,Mwambene
amevitaka vyombo vya habari nchini kufanya utafiti na kusoma kabla ya
kuandika habari na pia akaviasa kuandika habari zenye lengo la kujenga
umoja na mshikamano badala ya kuandika habari zenye lengo la kuwagawa
Watanzania
No comments
Post a Comment