Eneo la tukio husika |
Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la
Johnson Muchunguzi amefariki dunia baada ya kuangukiwa na miamba ya mawe
alipokuwa katika shughuli za uchimbaji wa mchanga kwenye eneo la
machimbo yasiyo rasmi ya Rwome yaliyopo katika kata ya Kashai Manispaa
ya Bukoba.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo
wamesema kijana huyo pamoja na wenzake walikutwa na dhahama hiyo jana
majira ya asubuhi baada ya jiwe kubwa kuanguka na kumfukia wakati akiwa
katika shimo alilokuwa akichimbia mchanga.
Vikosi vya usalama pamoja na kuwahi
katika eneo la tukio havikuweza kuokoa maisha ya kijana huyo ,ambaye
tayari alikuwa keshapoteza maisha kutokana na kuzidiwa na uzito wa jiwe
moja lililomgandamiza kabla ya kufuatiwa na jiwe jingine lililokatisha
tamaa juhudi za kumuokoa zilizokuwa zikifanywa na vikosi vya usalama
pamoja na wananchi.
Baadhi ya Wananchi walioshuhudia pamoja
na majirani wanaelezea kwa huzuni tukio hilo na kudai kuwa kijana huyo
alikandamizwa na jiwe kubwa ambalo lilikuwa lizito kwan walipofika eneo
la tukio walimkuta bado ni mzma akiomba msaada na kusema tukio hilo
limewahuzunisha sana.
Katika hali ya kushangaza Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Rwome Ponsian Wamala anakiri kuwepo kwa machimbo
hayo yasiyo rasmi,huku akishindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya
wachimbaji hao.
Hadi chanzo cha habari hii kinaondoka
katika eneo hilo bado juhudi mbalimbali zilikuwa zikiendelea kujaribu
kuutoa mwili wa marehemu Johnson kutoka katika shimo hilo.
No comments
Post a Comment