Msanii wa muziki wa Pop nchini Marekani, Janet Jackson ndugu yake mfalme wa pop duniani Marehemu Michael Jacksson Janet Jackson anatokea kwa mara nyingine katika stori za burudani siku ya leo.
Je, unafahamu kuwa Janet Jackson ana jumla ya Album 7 toka aanze kufanya muziki miaka ya ’80? na je unajua ni album zake ngapi zimeshawahi kushika #1 moja kwenye chati ya Billboard 200 ya Marekani? kama hufahamu basi ichukue hii hapa…
Janeth Jacksson ameibuka kwenye nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200 na ulbum yake mpya kabisa ‘Unbreakable’ ambayo ni album ya kwanza ya Janet baada ya kimya kingi kwa muda wa miaka 7, sio hayo tu… Billboard imemtaja Janet Jackson kama msanii wa tatu wa kike kuwa na Album 7 zilizoshika #1 ndani ya miaka 40!… kwa mujibu wa mtandao wa Billboard na Nielsen Music, album mpya ya Janet Jackson ilitoka tarehe 2 October 2015 na ndani ya wiki ya kwanza tu album hiyo ilifanya mauzo ya juu sana!Hii ni audio Album ya kwanza ya Janet Jackson toka Album yake ya mwaka 2008 ‘Discpline’ambayo pia kwa mujibu wa Billboard, Album hiyo iliibuka kwenye nafasi ya #1 kwenye chati ya Billboard 200…
Album nyingine za Janet Jackson zilizowahi kushika nafasi hiyo ni; All For You (2001), The Velvet Rope (1997), Janet. (1993), Janet Jackson’s Rhythm Nation 1814 (1989) na Control (1986).
No comments
Post a Comment