Alexis Sanchez wa Arsenal wa pili kulia akiruka juu kushangilia goli la kwanza alilofunga katika mchezo huo (katika ushindi wa magoli matatu kwa sifuri |
Arsenal leo wameamua kuinyamazisha Man United mapemaaa baada ya kutumia dakika saba sekunde 33 pekee baada ya goli la kwanza katika uwanja wake wa Emirates.
Alexis Sanchez alianzisha tabia mbaya hiyo ya kuwaaibisha mashetani hao mnamo dakika ya 6, huku mesut Ozil akiweka goli la pili dakika ya 7 kabla ya Sanches kuongeza goli la 3 dakika y a19 na kukamilisha ushindi huo mnono kabisa kwa timu hiyo.
Petr Cech alifanya juhudi kubwa kuzuia mashambilizi na mashuti ya washambuliaji wa manchester united wenye uchu wa kufunga kama Anthony Martial katika nusu ya kwanza ya mchezo na kipindi cha pili pia licha ya kushindwa kufua dafu na matokeo yakabaki hivyo hadi mwisho wa mechi.
No comments
Post a Comment