Ndege za kivita za Urusi zimehujumu kwa mara nyengine tena vituo vya
waasi nchini Syria.
Lengo lilikuwa vituo vya wanamgambo wa itikadi kali wa dola ya kiislam-IS-amesema msemaji wa wizara ya ulinzi mjini Moscow.
Urusi imeweka zaidi ya ndege za kivita na helikopta 50 nchini Syria.
Wadadisi wanaituhumu Urusi kuhujumu vituo vya waasi wa kutoka upande wa upinzani wanaofuata msimamo wa wastani.
Moscow lakini inakanusha tuhuma hizo.
Wanaharakati wa Syria wanazungumzia kuhusu hujuma za angani za Urusi katika eneo la kaskazini ya nchi hiyo,karibu na mji wa Idlib.
Urusi imeanza jana hujuma zake za angani kwa lengo la kuwasaidia wanajesahi watiifu kwa rais Bashar al Assad.
Iran imesifu uamuzi huo wa Urusi.
Urusi sawa na jamhuri ya kiislam ya Iran wanamuunga mkono rais Bashar al Asaad.

No comments
Post a Comment