Na. Peter Mkwavila,Mpwapwa.
WANAWAKE wilayani Mpwapwa wameliomba jeshi la polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha ulinzi wakati wote wa zoezi la kupiga kura na hata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu unaofanyika kesho
Hayo wameyasema wakati walipokuwa wakizungumza katika mjadala wa siku moja uluioandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Women wake Up (WOWAP) kupitia mradi wa Fahamu Ongea sikilizwa unaofadhiliwa na Oxfam.
Walisema kuwa wanawake wamekuwa wakipata hofu ya vuruigu baada ya matokeo kutangazwa ambapo baadhio ya viongozi wasipopita katika nafasi zao huanza kufanya vurugu huku waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.
Mmoaja wa wanake hao, Mary Madelemu alisema kuwa hivi sasa wanapewa vitisho na waume zao hivyo miongoni mwa wanawake wanaweza kuogopa kwenda kupiga kura jambo ambalo alisema kuwa litawanyima haki yao ya kidemkrasia ya kuchagua au kuchaguliwa.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ni vema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha kuwa wanaimarisha ulinzi wakati wote wa uchaguzi na hata baada ya matokeo kutangazwa.
Wanawake hao walisema kuwa mbali na kupata elimu ya kutosha ya masuala mazima ya uchaguzi lakini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa waume zao ambao hivi sasa wanadai kuwa siku ya uchaguzi lazima waambatane na wake zao ili waone wanakipigia kura chama gani.
"Nisema kwa sisi wanawake wa wilaya hii ya Mpwapwa baadhi yetu tumekuwa tukipata vitisho kutoka kwa wanaume zetu kuwa siku ya kupiga kura lazima tuambatane nao ili wakatusaidie namna ya kupiga kura jambo ambalo tunaona kuwa wanataka kutubana ili tuweze kuchagua viongozi wanaowataka wao."alisema
Mbali na changamoto hiyo lakini pia wanawake wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya majukumu ya nyumbani jambo ambalo alisema kuwa kwa siku hiyo lazima wanawake waanze kufanya maandalizi mapema ya kazi zao ili Octoba 25 wasiwe na kazi za kuwanyima fursa ya kwenda kuchagua viongozi wao.
Kwa upande wake naye Grace Chiyongo kutokana kata ya Nhgambi alisema kuwa kukandamizwa kwa wanawake wilayani huku kunatokana na mira na desturi jambo ambalo alisema kuwa mashirika na taasisi mbali mbali yanaowajibu wa kuendelea kutoa elimu ili jamii iweze kubadirika.
Alisema kuwa katika kata yao hakuna hata mwanamke mmoja aliyejitokeza na kugombea nafasi yoyote ya uongozi kutokana na baadhi ya wanaume katika eneo hilo kuwanyima fursa wake zao na kudai kuwa wakienda kugombea nafasi hizo za uongozi watafanya anasa.
No comments
Post a Comment