Viwango vya uchafuzi wa hewa huko
mjini Delhi nchini India vimeongezeka pakubwa hasa wakati wa usiku wa
sherehe za jamii ya Wahindi, sherehe za Diwali, vikifikia mara 40 zaidi
ya viwango vinavyopendekezwa na wataalam wa kimataifa, hayo ni kwa
mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
Kwa mfano Jumatano usiku vilifikia kiwango cha chembe chembe PM10 katika eneo lililopimwa ambacho ni hatari sana.
Kabla ya sherehe kuanza serikali ilikuwa imetoa wito watu wasitumie fataki katika sherehe hizo.
Gazeti la The Times of India hapo Jumatano lilikuwa limeripoti kuwa hali ya hewa imekuwa mbaya sana.
Viwango vya kemikali ya sulphur dioxide, ambayo inajulikana kuchochea pumu na maradhi mengine ya kupumua nayo pia ilikuwa ilikuwa juu katika maeneo mengi.
Uchunguzi wa WHO wa mwaka 2014 uligundua kuwa kati ya miji 20 iliyo na viwango vikubwa vya uchafuzi wa hali ya hewa duniani, 13 iko katika taifa la India, huku mji wa Delhi ukitajwa kushikilia nafasi ya kwanza ya miji iliyona uchafuzi zaidi wa hewa duniani.
No comments
Post a Comment