Jeshi la Polisi mkoani Tanga
limefanikiwa kukamata shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi kilo
462 iliyokuwa imehifadhiwa katika magunia aina ya viroba ikitokea Arusha
kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusambazwa kwa mawakala kwa
ajili ya kuuzwa kwa watumiaji.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga kamishna msaidizi wa Polisi Zubeir
Mwombeji amesema katika tukio hilo jeshi la Polisi limewatia mbaroni
watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na shehena ya hiyo ya mirungi na
kuwataja kwa majina kuwa ni dereva wa gari aina ya fuso lililokuwa
limehifadhi mirungi na Aloyce Gabriel mkazi wa picha ya ndege Kibaha na
Rashid Juma mkazi wa Mbauda mkoani Arusha.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wakielezea hatua hiyo wamesema
ili kudhibiti usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi ni
vyema askari wa jeshi hilo wakaimarisha doria sehemu za mipakani ambapo
wafanyabishara kutoka nchi jirani ya Kenya kwa kushirikiana na wenzao
waliopo katika vijiji vilivopo pembeni mwa bahari ya Hindi mkoani Tanga
wamekuwa wakipitisha bidhaa hiyo haramu kwa njia za panya pasipo
kukamatwa.
Kufuatia hatua hiyo kamanda Mwombeji amewataka wafanyabiashara
wenye magari ya mizigo na abiria kuachana na bishara ya kusafirisha dawa
za kulevya aina ya mirungi kwa sababu jehsi la polisi litataifisha
chombo cha usafiri kilichohusika na usafirishaji wa bidhaa hiyo haramu
kisha watuhumiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments
Post a Comment