Ndege za kivita za Marekani za B-52 zimepaa na kupitia katika eneo linalozozaniwa huko kusini mwa visiwa vya Uchina.
Zoezi hilo limefanyika licha ya onyo kutoka kwa maafisa wa Uchina.
Tukio hilo linafanyika huku ziara ya rais Barack Obama ya huko Manila ikitarajiwa wiki ijayo, ambako pia rais wa Uhina Xi Jinping anatarajiwa kuhudhuria.
Uchina inazozana pia na mataifa mengine kadhaa majirani zake katika eneo hilo la bahari.
Eneo hilo lina mali asili nyingi na Uchina inawahi kwa kujenga katika maeneo ya mwamba huo na kufanya harakati nyenginezo za kimaendeleo harakati zinazopingwa na majirani zake na hata Marekani.
Msimamo wa Marekani ni kuwa ingependelea kuwa na uhuru wa kupita maeneo hayo kwani ni kanuni za kimataifa kutomiliki meeneo ya bahari na anga yaliyombali sana na nchi yako.
Kwa msimamo huo wanasema kitendo cha kupelekwa kwa ndege hizo B-52 katika eneo hilo si kinyume cha sheria kama inavyodaiwa na Uchina kwani walikuwa umbali zaidi ya maili 15 ndani ya bahari kama inavyoruhusiwa na sheria za kimataifa.
No comments
Post a Comment