Bihar
Waziri mkuu wa jimbo la Bihar nchini
India ,Nitish Kumar ametangaza mipango ya kupiga marufuku uuzaji na
utumizi wa pombe katika jimbo hilo.
Hatua hiyo italigharimu jimbo la Bihar zaidi ya dola milioni 500 za kodi,kulingana na msemaji wa chama tawala cha Bihar Janata Dal.
Pombe imepigwa marufuku katika majimbo kadhaa ya India ikiwemo Gujarat na Manipur.
Bwana Kumar anaongoza muungano wa vyama vya kijimbo vilivyochukua mamlaka katika jimbo la Bihar mapema mwezi huu.
Wakati wa kampeni zake,alikabiliwa na maandamano ya wanawake ambao walilalama kuhusu ubugiaji mbaya wa pombe katika vijiji.
'Nahisi kwamba wanawake wanapata shinda zaidi ya wengine kutokana na unywaji wa pombe....nimeagiza maafisa wangu kuanza harakati za kupiga marufuku na kuanza kuidhinisha hatua hiyo kuanzia kipindi kijacho cha fedha,bwana Kumar alisema katika mkutano mwengine siku ya Alhamisi.
Mwaka uliopita,serikali kusini mwa Kerala ilitangaza mipango ya kuzuia uuzaji na unywaji wa pombe kwa mika 10.
Wamiliki wa baa na wale wa hoteli wamelipinga agizo hilo kwenye mahakama huku marufuku hiyo ikipunguzwa ili kuruhusu baa kuuza pombe na mivinyo.
Chanzo: bbcswahili
****************************************************************************************************
NAIROBI
Papa Francis amehutubia maelfu ya vijana nchini Kenya na kuwahimiza wasijihusishe na ufisadi na ukabila.
“(Ufisadi) Ni kama sukari, tamu, twaipenda, ni rahisi. Kisha, tunaishia kuumia. Sukari inaweza kuzidi hivi kwamba tunapata kisukari, au taifa letu linaishia kuwa na kisukari,” amesema.
"Nawasihi, msiipende sukari hiyo iitwayo ufisadi. Katika ufisadi, sawa na katika kila jambo, lazima uchukue msimamo. Ufisadi si njia ya uhai, ni njia ya mauti.”
Kadhalika, aliwahimiza wasijihusishe na ukabila na kuwataka wawatazame watu wengine kama raia wa taifa moja.
Papa Francis pia amewashauri Serikali zihakikishe vijana wanapata elimu na ajira, akisema ndiyo njia pekee ya kuwazuia kujiingiza katika makundi yenye itikadi kali.
Kwa mara nyingine, ameelezea umuhimu wa familia kama nguzo kuu katika jamii.
Maelfu ya vijana walikuwa wamejitokeza kwa hotuba ya Papa Francis na baadhi hawakupata nafasi ya kuingia ndani ya uwanja.
Awali, apotembelea mtaa duni wa Kangemi, alikemea unyakuzi wa ardhi na dhuluma wanazotendewa watu maskini mijini akisema wana haki sawa ya kupata huduma bora.
“Ninafahamu kuhusu tatizo kubwa linalosababishwa na wastawishaji wasio na sura ambao hujitwalia ardhi na hata kujaribu kunyakua viwanja vya kuchezea vya watoto wenu shuleni.
Hili ndilo hufanyika tunaposahau kwamba Mungu aliwapa watu wote ardhi, waitumie kwa maisha yao, bila kutenga au kupendelea yeyote," aliwaambia.
Papa Francis anatarajiwa kuondoka Nairobi baadaye leo kuelekea Uganda.
Chanzo: bbcswahili
********************************************************************************************************
JubaMakumi ya maelfu ya watu Sudan Kusini wanakabiliwa na hatari ya
baa kubwa la njaa wakati wa kuanza msimu wa kiangazi mwezi wa Januari.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Muungano wa Kimataifa wa Usalama wa Chakula IPC, jimbo la Unity pekee linaweza kukumbwa na maafa kwani watu 40,000 yamkini wakapoteza maisha kutokana na ukosefu wa chakula. Mwezi Oktoba shirika hilo lilisema watu 830,000 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula huku wengine milioni 3.1 wakikabiliwa na uhaba wa chakula.
Muungano wa kimataifa wa usalama wa chakula unajumuisha mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya umoja wa mataifa.
Machafuko ya ndani huko Sudan Kusini yaliibuka mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka 2013, baada ya Rais Salva Kiir, kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar kuwa alipanga njama za kutaka kumpindua.
Machafuko hayo yamesababisha maelfu ya watu kuuawa na maelfu ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
Licha ya kusainiwa makubaliano ya amani kati ya makundi hasimu nchini Sudan Kusini, bado kungali kunashuhudiwa machafuko, ghasia na mapigano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa waasi katika nchi hiyo.
Mapigano hayo yamepelekea kuvurugika kabisa shughuli za kilimo nchini humo.
Chanzo: iribswahili
****************************************************************************
MOSCOW
Rais wa Urusi, Vladmir Putin na mwenzake wa Ufaransa, Francois Hollande, wamekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi katika juhudi za kupinga ugaidi dhidi ya kundi lenye itikadi kali la Dola la Kiislamu-IS nchini Syria.
Wakati wa ziara ya Rais Hollande mjini Moscow jana, viongozi hao wawili walisema watashirikiana katika mashambulizi ya anga kwenye maeneo ya IS na kupeana taarifa za kijasusi kuhusu shughuli za kigaidi.
Putin amesema Urusi itafikiria kujiunga na jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani kufanya mashambulizi ya anga nchini Syria, lakini kama watakubaliana kuhusu mfumo wa kuendesha mashambulizi hayo dhidi ya IS.
Rais Putin pia ameitaka Uturuki iiombe radhi kutokana na kitendo chake cha kuishambulia ndege yake ya kijeshi mapema wiki hii.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius amesema anaona kuwa majeshi ya serikali ya Syria huenda yakashiriki katika mapambano dhidi ya IS.
Wakati huo huo Rais Putin amesema kitendo cha karibuni cha Jeshi la Anga la Uturuki cha kuitungua ndege ya Russia katika anga ya Syria kilikuwa ni cha usaliti kilichofanywa na nchi ambayo Moscow iliichukulia kuwa ni rafiki.
Chanzo: iribswahili
*************************************************************************

No comments
Post a Comment