Hivi karibuni kumetokea tafrani na kuwahusisha wakaazi wa jiji la Arusha, ambapo mwanaume mmoja wa washiriki wa mapenzi ya jinsia moja ilisemekana ni Raia wa Tanzania mkoani Arusha.
lakini Imethibitika kuwa mwanaume huyo shoga wa kiafrika aliyeonekana akivalishwa pete na mzungu ambaye ni raia wa sweeden anatokea nchini Uganda na siyo Tanzania kama ilivyoelezwa kwenye taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
kwa mujibu wa website ya kituo cha runinga cha CITIZEN cha nchini Kenya mwanaume huyo mwenye asili ya kiafrika aliwahi kuolewa na mwanaume mwenzake lakini alikimbia nchi ya Uganda baada ya kupitishwa kwa sheria dhidi ya watu wa aina yake sheria ambayo ilizua malumbano baina ya Uganda na mataifa ya magharibi.
vitendo hivyo vya ushoga vimekuwa ni vya kutisha kutokana na kutetewa sana na mashirika ya kutetea haki za kibinaadam huku vikipingwa na dini mbalimbali duniani isipokuwa baadhi ikiwemo uingereza kupitia kanisa la anglikan lililojitokeza wazi kuviunga mkono vitendo hivyo.
http://citizentv.co.ke
No comments
Post a Comment