Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuonya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin 'kutocheza na moto' kuhusu swala la taifa lake kuidungua ndege ya kijeshi ya Urusi.
Bwana Erdogan pia amesema kuwa anataka kukutana na bwana Putin ana kwa ana katika mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa ili kusuluhisha mzozo huo.Urusi imeamua kusitisha mpango wa kusafiri bila viza miongoni mwa raia wa mataifa hayo mawili kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
Uturuki inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa katika anga yake ilipolengwa,lakini Urusi inasema kuwa ilikuwa katika anga ya Syria.
''Ningependa kukutana na bwana Putin ana kwa ana mjini Paris'',alisema bwana Erdogan katika hotuba yake katika runinga.
''Ningependa kusuluhisha tatizo hili.Inaudhi kuona kwamba swala hili limeongezewa chumvi''.
Bwana Putin anataka kuombwa msamaha na Uturuki kabla ya kuzungumza na Erdogan ,msaidizi wa rais huyo amesema.
No comments
Post a Comment