Shirikisho la soka Duniani FIFA limeitaka TFF kuhakikisha klabu zote zinajiunga na mfumo wa GPX unaotoa taarifa zote za wachezaji
Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukiwataka mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers).
FIFA imeleta mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine lakini kabla ya kufanya hivyo utasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji huyo na shabaha kuu ni kurahisisha mawasiliano ya TMS Managers nchi nzima, klabu na mashirikisho mbalimbali duniani.
GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.
No comments
Post a Comment