******************************************************************************** |
NAIROBI
Waziri mwenye ushawishi mkubwa
katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya
shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na
tuhuma za ufisadi.
Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema.
CHANZO: bbswahili
*************************************************************************************************
SYRIA
Mkaazi mmoja wa ngome kuu ya
wapiganaji wa Islamic State huko Syria katika jiji la Raqq huku taarifa zikidai kuwa hali ya kibinadamu imezorota sana.
Alisema kuwa eneo kubwa la mji huo halina umeme na kuwa watu wanaotumia mitandao hawawezi tena kufanya hivyo.
Ilikuwa vigumu kwa raia kuondoa Raqqa kwa kuwa ni wanachama wa Islamic State pekee wanaoruhusiwa kuingia na kuondoka kupitia vizuizi vilivyoko vinavyozunguka mji wote.
*****************************************************************************************
PARIS
Vitendo vya chuki na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa vinaripotiwa kuongezeka siku baada ya siku hasa baada ya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris.
Makundi mawili ya kutetea haki za binadamu nchini Ufaransa yametangaza kuwa, vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini humo vimeshadidi baada ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris.
Abdallah Zekri Mkuu wa Kituo cha Kupambana na Vitendo vya Kuuonesha Uislamu kuwa ni tishio amesema kuwa, vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini humo vimeongezeka na kwamba, kwa wiki kumekuwa kukiripotiwa kesi nne hadi tano za vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Yasser Louati msemaji wa kituo kingine cha kutetea haki za Waislamu nchini Ufaransa na kupambana na vitendo vya kuufanya Uislamu uogopwe amesema kuwa, baada ya mashambulio ya kigaidi ya Paris kumeripotiwa makumi ya kesi za utumiaji mabavu dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo.
Ufaransa ina Waislamu milioni tano ambao wanaunda asilimia nane ya wakazi wa nchi hiyo.
chanzo: iribswahili
*******************************************************************************************************
South Island
Polisi wa New Zealand wanasema kuwa watu wote saba walioabiri ndege iloanguka katika kisiwa cha South Island wamefariki.
Helikopta nne zimetumwa eneo hilo kwa uwokozi na kutafuta mabaki ya ndege.
Shughuli hizo zimekuwa ngumu kwa sababu ya milima na mabonde.
Miaka mitano iliyopita ndege iliyokuwa imebeba waruka mwavuli ilianguka baada ya kupaa angani kutoka Fox Glacier na kuwaua watu tisa.
Chanzo: bbcswahili
********************************************************************
BEIRUT
Moussa Abu Marzook mjumbe mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, Wapalestina wana adui mmoja tu ambaye ni utawala wa Israel ambao watu wanapaswa kukabiliana nao.
Akizungumza katika Kongamano la kuunga mkono Intifadha ya Quds ya taifa la Palestina huko Beirut Lebanon, Moussa Abu Marzook amesema kuwa, Intifadha ya Quds imethibitisha kwamba, taifa la Palestina daima lipo uwanjani na kuna adui mmoja tu ambaye ni utawala vamizi wa Israel na hivyo kuna haja ya kupambana naye.
Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema bayana kwamba, Intifadha ya sasa ambayo lengo lake ni kuzikomboa ardhi za Palestina kutoka katika makucha ya utawala vamizi wa Israel na kuwakomboa mateka wote wa Kipalestina kutoka katika magereza ya Israel imepelekea kuweko ulinzi na himaya kwa Quds na Msikiti wa al-Aqswa mkabala na hujuma za Wazayuni wavamizi.
Aidha amesema kuwa, mataifa ya Kiislamu na Kiarabu yanapaswa kuunga mkono Intifadha ya taifa la Palestina na kuchukua hatua za kuiimarisha na kuipa nguvu Intifadha hiyo.
Chanzo: iribswahiliMoussa Abu Marzook mjumbe mwandamizi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, Wapalestina wana adui mmoja tu ambaye ni utawala wa Israel ambao watu wanapaswa kukabiliana nao.
Akizungumza katika Kongamano la kuunga mkono Intifadha ya Quds ya taifa la Palestina huko Beirut Lebanon, Moussa Abu Marzook amesema kuwa, Intifadha ya Quds imethibitisha kwamba, taifa la Palestina daima lipo uwanjani na kuna adui mmoja tu ambaye ni utawala vamizi wa Israel na hivyo kuna haja ya kupambana naye.
Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema bayana kwamba, Intifadha ya sasa ambayo lengo lake ni kuzikomboa ardhi za Palestina kutoka katika makucha ya utawala vamizi wa Israel na kuwakomboa mateka wote wa Kipalestina kutoka katika magereza ya Israel imepelekea kuweko ulinzi na himaya kwa Quds na Msikiti wa al-Aqswa mkabala na hujuma za Wazayuni wavamizi.
Aidha amesema kuwa, mataifa ya Kiislamu na Kiarabu yanapaswa kuunga mkono Intifadha ya taifa la Palestina na kuchukua hatua za kuiimarisha na kuipa nguvu Intifadha hiyo.
*******************************************************************************************************
ANTALYA
Uturuki inamshikilia raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco kutokana na tuhuma za kuhusika na mashambulizi ya Paris.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Dogan la nchini humo Ahmet Dahmani mwenye umri wa miaka 26 anatuhumiwa kufanya kazi ya upelelezi ya kuchagua maeneo ya kushambulia, katika mashambilizi yaliyosababisha vifo vya watu 130.
ipoti zinasema mtuhumiwa sambamba na watu wengine wenye uraia wa Syria waliokuwa wakimsaidia kuingia katika mipaka ya Syria wanashikiliwa eneo la pwani la jiji la Antalya.
Katika hatua nyingine ndege 22 za kivita za Uturuki zimeyashambulia maeneo ya Chama cha Wafanyakazi cha Wakurdi (PKK) kaskazini mwa Iraq na kusini mashariki mwa Uturuki jana usiku, ikiwa operesheni ya hivi karibuni dhidi ya kundi hilo la waasi. Jeshi la Uturuki limesema limeyashambulia maeneo 23 ya PKK.
chanzo : dwswahili
No comments
Post a Comment