Ligi Kuu Hispania imeendelea tena leo November 21 kwa kuzikutanisha timu kadhaa kucheza mechi zao za muendelezo wa Ligi Kuu Hispania, miongoni mwa mechi zilizochezwa November 21 ni mchezo wa watani wa jadi kati ya Real Madrid dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Real Madrid na FC Barcelona kabla ya mchezo huu wa kihistoria kuchezwa walikuwa wamepishana kwa tofauti ya point tatu, Real Madrid wakiwa nyuma kwa kupoteza mchezo mmoja, huu ndio mchezo ambao kwa sasa una rekodi za kuangaliwa na watu wengi duniani. Licha ya kuwa Real Madrid wanaongoza kwa takwimu ya kumfunga FC Barcelona mara 92 kwa 89 hawakuweza kutamba katika uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo ulianza kwa FC Barcelona kupiga pasi nyingi kama kawaida yao na dakika ya 10 Luis Suarez akaanza kuwapa furaha mashabiki wa FC Barcelona duniani kote kwa kufunga goli la kwanza, wakati ambao Real Madrid wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo, Neymar akapachika goli la pili dakika ya 39 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.
hivi ndivyo magoli yalivyoingia..tazama video ya magoli manne>>>

No comments
Post a Comment