Kundi la IS lilisema lilihusika kwenye mashambulio hayo ya Paris yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Aidha, lilidai kuhusika katika kulipua mabomu Lebanon mwezi huu. Awali, lilikuwa limesema lilihusika kudungua ndege ya Urusi eneo la Sinai mwezi Oktoba, na kuua watu 224.
Azimio hilo la UN nambari 2249 linashutumu mashambulio ya hivi majuzi Sousse, Tunisia, na Ankara, Uturuki.
Hatua hiyo ilichukuliwa huku maafisa nchini Ubelgiji wakitangaza kiwango cha juu zaidi cha tahadhari Brussels, na kuonya huenda kukatokea shambulio.
Baadhi ya walioshambulia Paris walikuwa wamekaa Brussels.
Manusura pekee wa kundi hilo, Salah Abdeslam, bado anasakwa na anadaiwa kurejea humo.
Serikali ya Ubelgiji imesema mshukiwa mwingine ameshtakiwa kuhusiana na mashambuliano hayo, na kufikisha idadi ya walioshtakiwa nchini humo hadi watatu.
Baraza la Usalama la UN liliyataka mataifa wanachama kuangamiza “maeneo salama” ya IS na wapiganaji wengine ambayo yameundwa Iraq na Syria.
Azimio hilo pia linasisitiza kwamba mataifa yanafaa “kuongeza maradufu na kuendesha juhudi za kuzuia na kukabili mashambulio ya kigaidi kwa pamoja”.
Hata hivyo, haijagusa Sura VII ya UN ambayo huidhinisha kutumiwa kwa nguvu.
Ufaransa na Urusi zilisema tayari inaruhusiwa kutumia nguvu kwa sababu mataifa yana haki ya kujilinda.
Awali, maafisa wa Ufaransa walisema binamu wa mhusika mkuu wa mashambulio hayo ya Novemba 13 mjini Paris hakujilipua wakati wa operesheni ya polisi Saint Denis kama ilivyodhaniwa awali.
Hotel iliyoshambuliwa nchini Mali |
Watu wenye silaha wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Kiislamu walishambulia hoteli ya Radissom Blue mjini Bamako na kushikilia mateka watu 170.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha hakuna mateka zaidi wanaoshikiliwa.
Makundi ya Al-Qaeda Afrika Kaskazini na kundi jingine la al-Murabitoun yamedai kuhusika kwenye shambulio hilo.
Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu shambulio hilo.
Akiongea baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri, Rais Keita alisema watu 21 waliuawa kwenye shambulio hilo, wakiwemo washambuliaji wawili.
Ripoti za awali zilikuwa zimesema watu 27 waliuawa. Afisa wa UN, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema miili 12 ilipatikana ghorofa ya chini ya hoteli hiyo na miili 15 ghorofa ya pili.
Mmoja wa mateka waliouawa ni Geoffrey Dieudonne, mbunge aliyewakilisha jimbo la Wallonia nchini Ubelgiji.
Shirika la habari la serikali ya Uchina Xinhua linasema raia watatu wa Uchina ni miongoni mwa waliouawa. Marekani nayo ilisema raia wake mmoja aliuawa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Philip Hammond alisema Waingereza watatu waliokuwa hotelini humo wako salama.
Hoteli hiyo inamilikiwa na Wamarekani na hupendwa sana na raia wa kigeni.
Watu walioshuhudia shambulio hilo walisema wapiganaji hadi 13 waliingia kwenye hoteli hiyo wakiimba "Mungu ni Mkubwa!” kwa Kiarabu.
Kabla ya vikosi maalum kuingia humo, mdokezi mmoja aliambia shirika la habari la Reuters kwamba baadhi ya mateka walioweza kukariri vifungu vya Koran waliachiliwa.
Chanzo: bbcswahili
******************************************************
Polis nchini ubelgiji wapo katika tahadhari kubwa ya kushambuliwa na magaidi |
BRUSSELS
Taarifa hizo zilizotolewa na kituo cha taifa nchini humo kinachohusika na ufuatiliaji wa matukio ya hali ya hatari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo hicho ambacho kiko chini ya wizara ya mambo ya ndani nchini humo hatua zaidi za tahadhari za kiusalama zinahitajika kuchukuliwa ili kukabiliana na kitisho hicho.
Hatua hii inakuja ikiwa ni wiki moja tu baada ya mashambulizi ya mjini Paris nchini Ufaransa yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Chanzo: Dwswahili
****************************************************************
DEIR EZZOR
Kiasi ya watu 36 wameuawa hapo jana
katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Urusi na Syria katika
jimbo linalodhibitiwa na kundi la dola la kiisilamu la Deir Ezzor nchini Syria
katika Shambulizi linalo elezwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu
kuanza kwa mzozo nchini humo.
Kwa mujibu wa kundi linaloangalia haki
za binadamu nchini Syria watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika
mashambulizi hayo yaliyofanywa zaidi ya mara 70 yakilenga miji kadhaa ya
jimbo hilo la Deir Ezzor na maeneo ya ukanda wa mafuta .
Jimbo hilo linadhibitiwa zaidi na
wanamgambo wa kundi la dola la kiisilamu ukiondoa uwanja wa ndege unaotumiwa
na jeshi na maeneo kadhaa yanayoshikiliwa na serikali ya nchi hiyo.
Shambulizi hilo linakuja mnamo wakati
majeshi yanayoungwa mkono na Marekani yanayopambana dhidi ya kundi la dola la
kiisilamu jumatatu wiki hii yakidai kuyaharibu malori 116 yanayobeba shehena ya
mafuta kwa ajili ya matumizi ya kundi hilo mashariki mwa Syria.
Chanzo: Dwswahili
**********************************************************
Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa kikao mwezi ujao kitakachoshuhudia makundi ya waasi yenye silaha yakiungana na upande wa upinzani wa kisiasa nchini Syria ili kuwa na sauti ya pamoja katika kuelekea mazungumzo yenye lengo la kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo.
Mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura akizungumza na gazeti moja la Al- Hayat alisema Saudi Arabia iko tayari kuyakutanisha makundi hayo na siyo tu ya kisiasa bali pia makundi yenye silaha yanayopigana dhidi ya vikosi vya serikali ya Rais Bashar al-Assad.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Riyadhi nchini Saudi Arabia Desemba 15, mwaka huu utasaidia kujenga umoja miongoni mwa makundi ya upinzani na kuyawezesha kushiriki mazungumzo hayo yenye lengo la kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo kwa miaka mitano sasa ambao tayari umesababisha vifo vya watu 250,000.
Chanzo: Dwswahili
********************************************************
Duru kutoka nchini humo zinaarifu kuwa helikopta za uwokozi zimetumwa katika eneo liliko tokea ajali hiyo lililoko katika ukanda wa pwani nchini humo.
Helkopta hiyo iliyoanguka inadaiwa kumilikiwa na kampuni moja binafisi inayohusika na biashara ya usafirishaji watu wakiwemo watalii nchini humo.
Chanzo: dwswahili
No comments
Post a Comment