Njombe
Na John Banda
Emmanuel Masonga aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Njombe kusini |
CHAMA cha demokrasia na maendeleo
Chadema mkoa wa Njombe kimesema kuwa kimeanda nyaraka za kutosha tayari
kwenda mahakamani kwaajili ya kuitaka mahakama kutengua matokeo ya
ubunge jimbo la Njombe kusini ambalo alitangazwa mshindi kutoka chama
cha CCM Edward Mwalongo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka katika
mkutano wa kuunda kamati ya kushugulkikia kesi hiyo aliye kuwa mgombea
wa ubunge jimbo la Njombe Kusini Emanuel Masonga kupitia chama hicho
amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya nyaraka zikatazo enda kuwasaidia
mahakamani.
Masonga amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya ushadidi na
nyalaka 14 zitakazo wasaidia kuifanya mahakama itengue ushindi
uliotangazwa na Tume ya uchaguzi kwa kumtangaza Mwalongo kuwa mshindi.
Mgombea ubunge wa jimbo la Njombe Kusini: Edward Mwalongo akijinadimbele ya wananchi |
Amesema kuwa wakazi wa Jimbo lake la Njombe kusini
wamejitolea kuhakikisha kuwa wanachangia gharama za kuendesha kesi hiyo
itakapo anza mpaka itakapo fikia ukomo.
Amesema kuwa wanaenda mahakamani kupinga uteuzi aliouita ni
batili uliotangazwa na Mkurugezi na kumtangaza yeye kuwa mshindi ama
kuruduwa kwa uchaguzi katika jimbo hilo la Njimbe Kusini ili kutangazwa
mshindi harali.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati waliyounda kwaajili ya
kushughulikia kesi hiyo Emmanuel Filangali alisema kuwa tayari vidhibiti
vya kesi hiyo vimekusanywa na kupewa mawakili wao kwaajili ya kwenda
kuisimamia kesi hiyo.
Hata hivyo chama hicho kinaziara ya jimbo zima kwaajili ya
kuwaeleza wanachama wake katika mikutano ya ndani juu ya nini chama
kinaenda kufanya huhusiana na ushindi wanao dai wamepokonywa.
No comments
Post a Comment